Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dk Mwinyi atengua uteuzi wa viongozi watano

Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi

Muktasari:

  •  Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi ametengua uteuzi wa viongozi katika Wizara za elimu, Uchumi na Uwekezaji na wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo.


Unguja. Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi ametengua uteuzi wa viongozi katika Wizara za elimu, Uchumi na Uwekezaji na wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.

Taarifa iliyotolewa na kusainiwa na Katibu Mkuu Mtendaji, Zena Said leo Februari 3, 2022 imewataja waliotenguliwa ni pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Utumishi na Uendeshaji Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, Omar Ali Omar.

Mwingine aliyetajwa katika taarifa hiyo ni Suleiman Yahya Ame Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu katika wizara hiyo ya elimu.

Wengine ni Fatma Iddi Ali, Kamishna wa Kazi katika ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji na Salum Ubwa Nassor, Ofisa Mdhamini, Wizara ya Habari Vijana, Utamaduni na Michezo, Pemba.

Katika orodha hiyo pia kuna Mkurugenzi wa Idara ya Jinsia na Watoto katika Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto, Nasima Haji Choum

Ametengua nafasi hizo kuanzia leo.