Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dk Mwinyi ateua makatibu wakuu sita

Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi

Muktasari:

Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi amefanya uteuzi wa makatibu wakuu sita baadhi wakibadilishwa wizara  na wengine kupandishwa  vyeo.

Unguja. Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi amefanya uteuzi wa makatibu wakuu sita baadhi wakibadilishwa wizara  na wengine kupandishwa  vyeo.

  

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na kusainiwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Zena Said leo Novemba 10, 2022 imesema Dk Islam Seif Salum ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais.


Kabla ya uteuzi huo Islam alikuwa Katibu Mkuu kazi na uwezeshaji katika ofisi ya Rais Kazi Uchumi na Uwekezaji.


Maryam Juma Sadalla ametuliwa kuwa Katibu Mkuu Kazi na Uwezeshaji katika ofisi ya Rais, Uchumi na Uwekezaji. Kabla ya uteuzi alikuwa katibu Mkuu wizara ya Maendeleo ya Jami, Jinsia Wazee na Watoto.


"Ali Khamis Juma ameteuliwa kuwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda, kabla ya uteuzi Ali alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali," imesema taarifa hiyo


Mwingine ni Abeida Rashid Abdallah ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto ambapo alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo.


Khamis Abdulla Said ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, kabla ya uteuzi huo alikuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, vijana utamaduni na michezo.


Saleh Juma Mussa ametuliwa kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu, awali alikuwa Ofisa Mwandamizi katika ofis ya Rais.


Thabit Idarous Faina ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa uchaguz time ya Uchaguzi, kabla ya uteuzi huo Faina alikuwa Katibu Mkuu ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais.


Viongozi wote wataapishwa kesho Ijumaa Novemba 11, Ikulu  Zanzibar.