Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dk Mwinyi ateua wanane, atengua mmoja

Dk Mwinyi ateua wanane, atengua mmoja

Muktasari:

  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Mwinyi leo Jumanne Septemba 28, 2021 amefanya uteuzi wa viongozi katika taasisi mbalimbali za umma na kutengua uteuzi wa Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Barabara Zanzibar, Fauzia Sinde Hassan.


Unguja. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Mwinyi leo Jumanne Septemba 28, 2021 amefanya uteuzi wa viongozi katika taasisi mbalimbali za umma na kutengua uteuzi wa Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Barabara Zanzibar, Fauzia Sinde Hassan.

Dk Mwinyi amemteua Hassan Simba Hassan Kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Kurusha Maudhui (ZMUX) huku Hiji Dadi Shajak akiteuliwa kuwa Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni hiyo.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo Jumanne na Katibu Mkuu Kiongozi, Zena Said imeeleza Mwalim Ali Mwalim ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Michezo (BTMZ).

“Omar Salum Mohamed ameteuliwa kuwa Kamishna wa Utamaduni katika Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo na Suleiman Abdulla Salim ameteuoliwa kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Utangazaji,” imeeleza taarifa hiyo.

Ali Haji Mwadini ameteuliwa kuwa Mhariri Mtendaji wa Shirika la Magazeti, na Robert Laurian Mweiro ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Mifumo ya Tehama katika ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

Taarifa hiyo pia imemtaja Ali Khamis Mohamed ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Manispaa Unguja.