Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dk Nchimbi: Hatutasita kuikosoa, elekeza Serikali

Katibu Mkuu wa CCM akizungumza kwa simu na  Waziri wa Maji, Jumaa Aweso katika mkutano wa hadhara uliofanyika Namanyere mkoani Rukwa.

Muktasari:

Chama cha Mapinduzi (CCM), kimesema hakitasita kuikosoa,kuielekeza  Serikali kwenye mapungufu ili taasisi hizo kuwa na lengo moja ya kufanikisha maendeleo ya nchi

Rukwa. Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk Emmanuel Nchimbi amesema chama hicho, kitaendelea kutimiza majukumu yake ikiwamo kutosita kuikosoa Serikali ili kujirekebisha kwenye upungufu, akiwataka Watanzania kukiunga mkono.

Dk Nchimbi ameeleza hayo leo Jumapili Aprili 14, 2024 wakati akizungumza katika mkutano wa hadhara na wananchi wa Nkasi mkoani Rukwa katika mkutano wa hadhara uliofanyika stendi ya mabasi ya Namanyere ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya mikoa sita akianzia Katavi juzi.

Katibu mkuu huyo amesema chama hicho kinadhamira ya dhati na viongozi wanaoweza kutelekeleza dhamira hiyo ya kuondoa umasikini kwa wananchi.

"CCM itatekeleza kwa nguvu zote katika kuhakikisha Serikali inawatumikia wananchi kwa nguvu zote, hatutasita kukosoa, kuelekeza lakini wote tukijikita katika kufanikisha maendeleo ya nchi yetu," amesema Dk Nchimbi.

Ampigia simu Aweso

Katika hatua nyingine, Dk Nchimbi alimpigia simu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso akimataka kujua lini Serikali itapeleka Sh400 milioni zilizobaki kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa maji wilayani Nkasi.

Hatua hiyo, ilikuja baada ya mbunge wa Nkasi Kusini (CCM), Vicent Mbogo kueleza wilayani humo kuna changamoto mbalimbali ikiwemo upatikanaji wa maji safi akisema awali Serikali ilipeleka Sh300 milioni kati ya Sh700 milioni zilizobaki kwa ajili ya kutekeleza mradi wa maji.

Hata hivyo, kabla ya kujibu kero hiyo, Dk Nchimbi amesema akiwa ameketi meza kuu aliwasiliana na Aweso kutaka kujua ahadi ya kumalizia Sh 400milioni zilizobaki, ndipo alipopanda jukwaani kuhutubia akiwaambia wanaNkasi kuwa anampigia tena simu waziri huyo ili wamsikie.

Dk Nchimbi amesema Rais Samia ameteua watu makini katika wizara zinazogusa matatizo ya wananchi ikiwamo wizara ya maji inayoongozwa na Aweso ambaye ni kijana mchapakazi anayeweza kuangaika na kero za wananchi.

Akijibu kero hiyo, Waziri Aweso amesema Sh400 milioni zilizobaki zitapelekwa wakati wowote kuanzia kesho Jumatatu Aprili 15, 2025 akisema atamuelekeza katibu mkuu wake fedha hizo zitoke kukamilisha mradi huo wa maji.

"Maelekezo ya chama kwetu sisi ni utekelezaji nikuhakikishie katibu mkuu (Dk Nchimbi), wizara ya maji haitakuwa kikwazo cha kuhakikisha dhamira ya Rais ya kumtua mama ndoo kichwani inatekelezeka," amesema Aweso.

Baada ya kukata simu ya Aweso, Dk Nchimbi amesema:"Hawa ndio aina ya mawaziri tunaowataka, sio unapata waziri mmoja hajiamini unamwambia lete Sh400milioni anakwambia ooh katibu mkuu kwanza sijala inatuhusu nini tunataka mtu anayejua kazi yake," amesema.

Dk Nchimbi ametumia nafasi hiyo kuupongeza mkoa wa Rukwa kwa kuwa ni miongoni mwa wachapa kazi katika shughuli za kilimo na kuwa mikoa mitano bora ya uzalishaji mazao ya chakula na kulisha Tanzania na mataifa ya jirani.


Rais Samia

Katika hatua nyingine, Dk Nchimbi amesema Rais Samia Suluhu Hassan ni kiongozi msikivu na mchapakazi akitolea mfano namna alivyoamua fedha za mkopo za Uviko-19 zitumike katika kuboresha huduma za kijamii ikiwamo zahanati,vituo vya afya na shule.

"Nchi nyingi za Kiafrika zilizopewa fedha hizi, viongozi walizitumia kugawana kununua magari ya kifahari, lakini Tanzania Rais Samia akasema zitumike kujenga hospitali, shule na kununua vifaa tiba, zote zilitawanywa mikoani haikubaki hata senti moja Ikulu.

"Mama Samia tumpe maua yake kwa wananchi angekuwa mroho angekusanya na kuzigawanya kwa watoto, ndugu na marafiki zake," amesema.

Amesema hivi sasa watu wana uhuru wa kuongea, akiwataka Watanzania kutumia vema uhuru huo kwa kutodhalishana, kuvunjiana heshima, kuongea kwa upendo na kushinda kwa hoja badala ya kebehina matusi.

Awali, Katibu wa Itikadi,Uenezi na Mafunzo wa chama hicho, Amos Makalla amewataka wananchi wa Nkasi kujipanga kwa ajili ya maandalizi ya chaguzi zijazo ukiwamo wa uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji na uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

Makalla amesisitiza katika mikutano yao hadhara watasikiliza kero lakini ziwe za kweli, zisizo na fitina au jambo hilo kuwepo mahakamani kwa sababu CCM wanaheshimu mhimili huo.

Mwenyekiti wa CCM, mkoani Rukwa Silafu Maufi amesema Wilaya ya Nkasi ina majimbo mawili na kata 20 kati ya hizo tano zipo upinzani. Amesema watahakikisha CCM inanyakua kata hizo kwa kutatua changamoto zinazowakabili wananchi.

"Naomba viongozi wetu wa CCM na Serikali tusikilize maelekezo na kuyafanyia kazi," amesema Maufi.