Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Fidia waliopisha mradi wa Liganga, Mchuchuma mwezi huu

Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Anthony Mtaka.

Njombe. Wananchi waliopisha mradi wa Liganga na Mchuchuma wilayani Ludewa mkoani Njombe wanatarajiwa kulipwa fidia zao Juni 7, 2023.

Hayo yamesemwa leo Jumatatu Juni 5, 2023 na Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Anthony Mtaka wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapa.

Amesema wananchi watakaolipwa ni waliofanyiwa tathmini na kuhakikiwa taarifa zao ambao wanatoka katika vijiji vya Mkomang'ombe, Amani pamoja na Mundindi.

Amesema Rais Samia Suluhu Hassan ameielekeza Wizara ya Fedha na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kulipa fidia hizo kwa wananchi.

Amesema zoezi hilo la ulipaji uzinduzi wake utafanyika Jumatano Juni 7 kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa ambapo walengwa wote ambao majina yao yapo kwenye fidia wanakaribishwa.

"Tunafanya hivi kwa uwazi kwasababu kumekuwa na tabia ya Serikali kufanya malipo ya fidia lakini baadae wananchi wanasema fidia haijalipwa," amesema Mtaka.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC), Nicolaus Shombe amesema jumla ya kiasi kitakacholipwa kama fidia kwa wananchi hao waliopisha mradi ni Sh15.4 bilioni.

Amesema wanufaika watakaolipwa fidia kutokana na kupisha mradi huo wa Liganga na Mchuchuma ni 1,142 ambapo inahusisha wananchi pamoja na taasisi.

"Hili zoezi tulianza tangu Aprili watu wote walihakikiwa na kusaini fomu za kukubali kiasi ambacho wanakwenda kulipwa," amesema Shombe.