Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Filamu ya Aisha yazoa tuzo nne Ziff

Muktasari:

  • Filamu ya Aisha iliyotayarishwa na Chande Othman imefanikiwa kushinda tuzo nne usiku kupitia tuzo ya mtayarishaji bora Bongo Movie, Mwigizaji bora wa kike ni Godliver Gordian aliyeigiza kama Aisha,  Best Feature Film ni Godliver Gordian na mwongozaji bora ni Amil Shivji kupitia filamu ya Aisha.

Zanzibar. Tuzo za filamu kupitia Tamasha la Kimataifa la filamu la nchi za majahazi (Ziff),  zimetolewa usiku wa kuamkia leo huku filamu ya Aisha ikizoa tuzo nne kupitia Bongo Movies.

Filamu ya Aisha iliyotayarishwa na Chande Othman imefanikiwa kushinda tuzo nne usiku kupitia tuzo ya mtayarishaji bora Bongo Movie, Mwigizaji bora wa kike ni Godliver Gordian aliyeigiza kama Aisha,  Best Feature Film ni Godliver Gordian na mwongozaji bora ni Amil Shivji kupitia filamu ya Aisha.

Filamu nyingine iliyochukua tuzo tatu ni filamu ya A Place For Myself, iliyoandaliwa na Clementine Dusambejambo kutoka Rwanda ambayo imechukua filamu kutoka Afrika Mashariki, filamu fupi bora na pia imepata Tuzo ya East Africa Talent.

Filamu nyingine iliyojichukulia umaarufu ni pamoja na Watatu ya Nick Reding na David Kinyanjui kutoka Kenya iliyochukua Tuzo ya European African Film Festival Award.

Signis Award imekwenda kwa filamu ya Me Belgium and My Mother are Ghanaian, A Place For Myself, Watatu ya Nick Reding (Kenya).

Tuzo ya Sembene Ousmane Award zimekwenda kwa The Suit /Jarryd Coestsee toka Afrika Kusini, Zawadi /Richard Card, David Kinyanjui - Kenya,  A Place For Myself imeandaliwa na Clementine Dusambejambo /Rwanda, Macarrao/Iyabo Kwayana-Brazil na filamu ya Ugali The Family Dinner Iliyotayarishwa na Tony Koros toka Kenya ambapo washindi wote wametunukia Dola za Marekani 2000.

Tuzo ya Emerson Zanzibar Foundation imekwenda kwa filamu ya Daladala iliyoandaliwa na Salum Stika kutoka Tanzania.

Salum amepewa Tuzo iliyoambatana na zawadi ya Dola za Marekani 1000

Bongo Movies Awards

Filamu za Bongo Movie kwa mwaka huu zimekuwa ni mbaya kwa mastaa wa Bongo Movie ambao wameondoka mikono mitupu huku Tuzo nyingi zikichukuliwa na waigizaji wachanga.

Filamu ya mwigizaji bora wa kiume imekwenda kwa Salim Ahmed 'Gabo'  kupitia filamu ya Safari ya Grand.

Mwandishi bora wa filamu kwa mwaka huu ni Abubakar H Guni na Devotha Mayunga kupitia filamu ya Queen of Maasai.

Tuzo hii pia ilishinda tuzo ya AMVCA mwaka huu na Richie alichukua Tuzo Nigeria.

Tuzo ya Bongo na Flava imekwenda kwa Joseph Myinga huku mtayarishaji bora ikienda kwa Chande Othman kupitia filamu ya Aisha.

Mpiga picha bora wa filamu ni Freddy Feruzi kupitia filamu ya Kariakoo na mhariri bora Momose Cheyo kupitia filamu ya Aisha.

Mwigizaji bora wa kike ni Godliver Gordian kupitia filamu ya Aisha ambaye pia amechukua Best Feature Film.

Lifetime Achievement Award  imekwenda kwa Mzanzibar ambaye amefanya shughuli nyingi za kijamii, lakini pia ni mbunifu wa mitindo aliyewahi pia kumvalisha Queen Elizabeth wakati akifanya shughuli zake za ubunifu kwa miaka 18 nchini Uingereza / Farouque Abdela.

Tuzo ya Bi Kidude iliyoandaliwa na Mandlakayse Dube imekwenda kwa filamu ya Kalushi kutoka Afrika Kusini.

Tuzo za Ziff zimekwenda kwa filamu ya Adam Mensch kutoka Belgium iitwayo Me a Belgian My Mother a Ghanaian.

Filamu bora fupi ya Ziff imekwenda kwa

A Place For Myself iliyoandaliwa na Clementine Dusambejambo /Rwanda.

Best Documentary - silver Dhow imekwenda kwa The Valley of Salt ya Christopher Saber, filamu bora iliyochukua Tuzo ya dhahabu ni Watatu ni ya Nick Reding kutoka Kenya.

Mwaka huu Ziff imetoa Tuzo kwa video bora ya muziki ya msanii iliyofanya vizuri Afrika Mashariki ambayo ni Walk It Off ya Fid Q feat TAZ.

Tamasha la Ziff 2017 linatarajiwa kuanza, Julai 8 mpaka 16 na litakuwa na kauli mbiu isemayo 'Finding Joy'  au  'Kusikia Furaha'.