Gambo amtumia ujumbe Lema

What you need to know:

Mbunge wa Arusha Mjini (CCM), Mrisho Gambo amemkaribisha mpinzani kwake kwenye siasa za jimbo hilo, Godbless Lema nchini Tanzania akisema, “siasa za ushindani zina raha yake.”


Dar es Salaam. Mbunge wa Arusha Mjini (CCM), Mrisho Gambo amemkaribisha mpinzani kwake kwenye siasa za jimbo hilo, Godbless Lema nchini Tanzania akisema, “siasa za ushindani zina raha yake.”

Gambo ametoa kauli hiyo ya leo Jumatano, Machi 1, 2023 kupitia ukurasa wake wa Twitter akiweka picha waliyopita pamoja na Lema na kuandika, “karibu nyumbani Mhe Godbless Lema.”

“Siasa za ushindani zina raha yake. Karibu tufanye siasa za kistaarabu Jijini Arusha! Kazi zinaendelea!”

Gambo na Lema wamekuwa katika mchuano wa kisiasa kwa kipindi kirefu, kuanzia kipindi Lema akiwa Mbunge wa Arusha Mjini huku Gambo akiwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

Katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 2020, Gambo alishinda uchaguzi huo dhidi ya Lema wa Chadema ambaye baada ya uchaguzi huo Lema alidai kutishiwa maisha na kuamua kutimkia Nairobi Kenya na baadaye kutimkia Canada.