Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

GCLA yatakiwa kusimamia usalama wachimbaji wadogo

Meneja wa GCLA Kanda ya Kusini Mtwara Hadija Mwema

Muktasari:

  • Mkuu wa Wilaya ya Lindi Shaibu Ndemanga, amewataka Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA), kusimamia wachimbaji wadogo wa madini kwa kuwafuata na kutoa elimu migoni.

Ruangwa. Mkuu wa Wilaya ya Lindi Shaibu Ndemanga, amewataka Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA), kusimamia wachimbaji wadogo wa madini kwa kuwafuata na kutoa elimu migoni.

Ndemanga amesema hayo jana Agust 25, 2023 mjini hapa, kwenye maonesho ya madini na uwekezaji, huku akisema GCLA ina wajibu wa kusimamia wachimbaji wadogo katika kuimarisha uchimbaji na usalama wa wachimbaji.

“Nendeni kwenye migodi...wahini mapema kwenye maeneo ya wachimbaji wadogo, pamoja na kutoa elimu kwenye migodi na pia mtasaidia kuimarisha uchimbaji na hivyo kuwa endelevu, lakini pia kuhakikisha wakati wote, usalama wa wachimbaji unazingatiwa,” amesema DC huyo.

Aidha, Meneja GCLA Kanda Mtwara, Hadija Mwema, amesema kuwa wataendelea kuwakagua lakini pia kutoa elimu juu ya matumizi bora ya kemikali salama.

"Tumelipokea tutalifanyia kazi kwa kuendelea kutoa elimu kwa wachimbaji, kuwasajili na kuwakagua ili kuweza kutumia kemikali salama kwaajili ya afya yao,” amesema Hadija.

Hata hivyo Mkurugenzi wa GCLA kanda hiyo, Daniel Mndio, amesema kuwa lengo walilokuwa nalo ni kushirikiana, na Tume ya Madini kwa kusajili mwalo yote, ambayo inatumika katika uchenjuaji wa madini, kwa kutumia Zebaki na kujua matumizi yake kama yanatumika kwa usahii.

"Lengo, ni kushirikiana na Tume ya Madini kwa kuthibiti mwalo yote, ambayo itatumika katika uchenjuaji wa madini kwa kutumia Zebaki"Amesema Ndalo.

 Mchimbaji mdogo wa  madini ya Namungo, Fadhili Kandala  amesema, GCLA ikiwatembelea  kwa kutoa elimu  ,itakuwa imewasaidia sana kwakuwa  wachimbaji wadogo wamekuwa hawajui usalama wao .

"Hawa GCLA wakija migodini kutupa elimu, kwakweli watakuwa wamefanya jambo jema, maana sisi kama wachimbaji hatujui kabisa usalama wetu, kwakuwa baadhi yetu sisi elimu haijatufikia," amesema Fadhili