Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gulio la Lindi kuchochea biashara na maendeleo ya wajasiriamali

Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Selemani Jafo.

Lindi. Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Selemani Jafo, ameliagiza Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) kutengeneza mashine za kuchakata mwani na kukamua mafuta ya ufuta kwa vikundi vya wajasiriamali wa Lindi kupitia Mfuko wa NEDF.

“Tunataka kuwa na viwanda vidogo vya kuongeza thamani kwenye bidhaa zetu,” amesema Waziri Jafo Novemba 2, 2024 alipokuwa akizindua Gulio la bidhaa za usindikaji na ushonaji linaloendelea Lindi, Novemba 1-3.

Akiwahimiza wajasiriamali hao kupata nembo ya ubora na "bar code" kwa ushirikiano na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO), Waziri Jafo alibainisha umuhimu wa bidhaa zao kushindana katika masoko ya kimataifa kama Jumuiya ya Afrika Mashariki na Eneo la Biashara Huria la Bara la Afrika (AfCFTA). Pia, alizindua Soko Mtandao (e-Soko), akielekeza kuwa gulio hilo lifanyike kila mwezi kwa ushirikiano na Tantrade ili kuvutia wajasiriamali.

Upande wake Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Zainab Telack, ameomba Serikali kusaidia viwanda vya kuchakata mazao kama ufuta na mwani, ambavyo ni malighafi za mkoa huo.

Aidha, Mzee wa Kimila wa Lindi, Abdallah Hamis Livembe, alimvisha Waziri Jafo vazi la kimila kama ishara ya utawala wa mkoa huo na kumwomba mkoa huo kupewa kipaumbele katika viwanda ili “kufuta jina la kuwa nyuma kimaendeleo,” amesema.