Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hakimu mbaroni akidaiwa kumlawiti bodaboda

Muktasari:

  • Jeshi la Polisi Wilaya ya Ngorongoro linamshikilia Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Loliondo, Mkoa wa Arusha kwa tuhuma za za kumlawiti kijana mwenye umri wa miaka 29.

Arusha. Linaweza kuwa ni moja  ya matukio ya nadra kutokea nchini, baada ya Jeshi la Polisi  kumtia mbaroni hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Loliondo, Mkoa wa Arusha kwa tuhuma za kumlawiti kijana mwenye umri wa miaka 29 baada ya kumlewesha pombe.

Mbali na hakimu huyo kushikiliwa,  jeshi hilo linamshikilia pia mwathirika wa tukio hilo kutokana na msimamo wa sheria unaosema kuwa  mwanamume anayemruhusu mwanamume mwenzake kumwingilia, naye ametenda kosa la jinai.

Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro (DC), Kanali Wilson Sakulo, amethibitisha kuwepo kwa tukio hilo.

"Ni kweli kuna taarifa za tukio la aina hiyo nimezipata na Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi, kwa sasa siko kwenye nafasi ya kusema tukio hilo," amesema.

Taarifa kutoka wilayani humo,  zinadai hakimu huyo anashikiliwa katika Kituo cha Polisi cha Loliondo.


Inadaiwa tukio hilo limetokea juzi Alhamisi, Februari 1, 2024 saa tatu na saa nne usiku nyumbani kwa kijana huyo ambaye hufanya kazi ya kuendesha bodaboda katika eneo la Wasso, wilayani Ngorongoro mkoa wa Arusha.

Chanzo hicho kilidai hakimu huyo ambaye hivi karibuni alihamia kikazi, alionekana majira ya mchana akiwa na kijana huyo na baadaye jioni walikwenda kunywa pombe nyumbani kwa kijana huyo.

"Ilipofika majira ya usiku kaka yake na kijana aliyelawitiwa (jina linahifadhiwa) alifika nyumbani kwa mdogo wake na kuwakuta wakiwa uchi, ndipo alipompigia simu hakimu mwenzake na mtuhumiwa," amedai mmoja wa chanzo chetu

"Alipokuja huyo Hakimu mwenzake, walipiga simu polisi na polisi walikuja kuwachukuwa wote wawili na hadi sasa wanashikiliwa kituoni," ameongeza

Chanzo hicho kiliendelea kueleza kijana huyo katika mahojiano ameeleza hii ni mara ya tatu hakimu huyo kumfanyia kitendo hicho na aliamua kunyamaza kwa madai aliona kutoa taarifa ingemdhalilisha na alipelekwa katika hospitali ya Wasso kwa matibabu na daktari kuthibitisha kuwa ameingiliwa.

"Kijana kwenye mahojiano alisema alikunywa sana pombe ikamzidi na kuamua kulala na aliposhtuka alikuta hakimu huyo akiwa anamwingilia kinyume na maumbile na kutokana na ukaribu wao hata kaka wa kijana alianza kuwa na mashaka," kilidai chanzo hicho

Taarifa zinadai hakimu hiyo alikuwa na mazoea na kijana hiyo kutokana na kumtuma mara kwa mara ikiwemo kumsafirisha kutoka eneo moja kwenda jingine kwa kutumia pikipiki yake.