Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hatimaye Henry apata ushindi

Muktasari:

Pengine mambo yakaanza kumnyookea kocha wa Monaco Thierry Henry, baada ya juzi kupata ushindi bao 1-0 dhidi ya Caen ukiwa ndio wa kwanza kwake tangu ameanza kuinoa timu hiyo Oktoba mwaka huu,

 


Paris, Ufaransa. Hatimaye Thierry Henry amepata ushindi wa kwanza tangu ateuliwa kuwa kocha wa timu ya Monaco, baada ya kuilaza Caen 1-0.

Mfaransa huyo, aliyeitumikia Monaco kwa mafanikio makubwa alipewa kibarua cha kuinoa timu hiyo wiki sita zilizopita, lakini tangu ameanza kazi hiyo hakupata ushindi zaidi ya sare mbili na kupoteza nne.

Bao lililompa matumaini mema Henry lilifungwa na Radamel Falcao, katika dakika ya 54 kwa mpira wa adhabu ukiwa ushindi wa kwanza kwa Monaco tangu Agosti 11.

Ingawa ushindi huo haujainasua timu hiyo iliyotwaa ubingwa wa msimu wa 2016/17 katika janga la kushuka daraja lakini umeipandisha kwa nafasi moja na kufufua morari kwa wachezaji.

Kabla ya kupewa kibarua hicho Henry, alikuwa kocha msaidizi wa timu ya Taifa ya Ubelgiji na alitwaa mikoba hiyo baada ya klabu kumtimua Leonardo Jardim, katikati ya Oktoba ikiwa nafasi ya tatu kutoka chini.

Aidha huo ulikuwa mchezo wa kwanza kwa Monaco kutofungwa bao tangu Agosti hata mechi ilizotoka sare ziliwa za mabao.