Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hili ndilo kosa la ugaidi aliloshitakiwa nalo mhadhiri wa UDOM

Muktasari:

  • Kaijage alifikishwa mahakamani leo, Alhamisi, Julai 23, 2026, mbele ya Hakimu Mkazi Zabibu Mpangule na kesi yake imeahirishwa hadi Agosti 5, 2026.




Dodoma. Baada ya kushikiliwa na polisi mkoani Dodoma kwa siku 15, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Melkisedek Kaijage, amefikishwa mahakamani mjini Dodoma, akishtakiwa kwa kosa la uhujumu uchumi la ugaidi.

Mhadhiri huyo alifikishwa mahakamani leo, Alhamisi, Julai 23, 2026, na kusomewa shitaka lake mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma, Zabibu Mpangule, na kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 5, 2026, itakapotajwa.

Kaijage alikamatwa Julai 8, 2026, akituhumiwa kuhamasisha maandamano yaliyokuwa yamepangwa kufanyika Julai 7, 2026, siku ya Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa (DITF) maarufu Sabasaba, ambayo kwa sehemu kubwa huadhimishwa jijini Dar es Salaam.

Jeshi la Polisi lilipiga marufuku kufanyika kwa maandamano hayo yaliyokuwa yakihamasishwa na wanaharakati kupitia mitandao ya kijamii, wakidai yangefanyika nchi nzima licha ya Jeshi la Polisi na Serikali kuyapiga marufuku.

Leo, Julai 23, 2026, mhadhiri huyo, aliyekuwa akishikiliwa katika Kituo cha Polisi cha Chang’ombe jijini Dodoma kwa tuhuma za kuhamasisha maandamano hayo, alifikishwa mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma kwa kosa la ugaidi.

Kosa aliloshtakiwa nalo linaangukia katika Kifungu cha 4(1), (2)(a) na (3)(c) cha Sheria ya Kuzuia Ugaidi, Sura ya 19, Toleo la Mwaka 2023, kikisomwa pamoja na Aya ya 24 ya Jedwali la Kwanza na Vifungu vya 57(1) na 61(2) vya Sheria ya Kudhibiti Makosa ya Uhujumu Uchumi na Uhalifu wa Kupangwa, Sura ya 200.

Upande wa mashtaka ulidai kuwa Julai 3, 2026, katika eneo la UDOM, anadaiwa kutenda kosa la kigaidi, ambalo ni kinyume cha sheria za Tanzania.


Kulingana na maelezo ya Jamhuri, anadaiwa kutishia kuchoma moto majengo ya umma na makazi ya polisi ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa lengo la kuwatisha wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa shtaka hilo, kwa mujibu wa sheria za Tanzania, linasikilizwa na Mahakama Kuu. Mahakama za chini hufanya mchakato wa kuhamishia shauri Mahakama Kuu (committal proceedings).

Mshtakiwa huyo ataendelea kushikiliwa mahabusu kwa kuwa kosa hilo halina dhamana.