Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hospitali ya Bugando sasa kupasua, kupandikiza koo bandia

Jopo la wataalam wa afya Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando jijini Mwanza likiongoza na Daktari Bingwa wa Upasuaji na Tiba ya Mfumo wa Chakula, Dk Ahmed Binde wakiendelea na upasuaji wa kuandikiza koo bandia kwa mgonjwa kumaliza tatizo la kushindwa kunywa na kula kutokana na maumivu ya koo. Picha na Mpiga Picha Maalum 

Muktasari:

Huduma hiyo ambayo tayari imemnufaisha Boniface Waryoba, mkazi wa Sengerema ambaye amepandikizwa koo bandi inafanyika kwa mgonjwa kupadikizwa kifaa maalum kwenye koo lenye uvimbe ama lililoziba, lengo ikiwa ni kumwezesha mgonjwa kula na kunywa bila maumivu.

Mwanza. Matumaini mapya yameanza kurejea kwa wagonjwa wa saratani ya koo, wenye uvimbe na makovu kooni waliokuwa na tatizo la kushindwa kunywa na kula kutokana na maumivu wakati wa kumeza chochote baada ya Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando ya jijini Mwanza kuanza kutoa huduma ya upasuaji wa kupandikiza koo la bandia (Esophageal Stent).

Huduma hiyo ambayo tayari imemnufaisha Boniface Waryoba, mkazi wa Sengerema ambaye amepandikizwa koo bandi inafanyika kwa mgonjwa kupadikizwa kifaa maalum kwenye koo lenye uvimbe ama lililoziba, lengo ikiwa ni kumwezesha mgonjwa kula na kunywa bila maumivu.

Upasuaji na upandikizwaji wa koo bandia unafanywa na jopo la madaktari bingwa wakiongozwa na Daktari Bingwa mbobezi wa Magonjwa ya Mfumo wa Chakula na Ini Hospitali ya Rufaa Bugando, Dk David Majinge.

Akizungumza na Mwananchi katika mahojiano maalum, Dk David Majinge amesema mara nyingi tatizo la kushindwa kumeza chakula na viminika huwakumba wagonjwa wa saratani ya koo, wenye uvumbe na makovu kooni.

Pamoja na saratani, uvimbe na makovu, mtaalam huyo ametaja unywaji wa pombe kali kwa mfumo wa kuchanganya aina tofauti za pombe maarufu kama kokteli kuwa miongoni mwa sababu zinazosababisha koo na njia ya chakula kuziba.

‘’Ni vema wananchi waepuke mifumo ya maisha yanayoweza kuwasababishia madhara ya kiafya ikiwemo unywaji wa pombe kali kwa mtindo wa kuchanganya aina tofauti kwa wakati mmoja,’’ amesema Dk Majinge

Akizungumzia upandikizaji wa koo bandia, Daktari Bingwa wa Upasuaji na Tiba ya Mfumo wa Chakula, Dk Ahmed Binde amewatoa wananchi hofu akisema hauna madhara yoyote kiafya kwa sababu hufanyika kwa kutumia vifaa maalum vyenye madini chuma yasiyo na athari kiafya.

‘’Nawasihi wote wenye maumivu ya koo, uvimbe, makovu na tatizo la kushindwa kumeza chakula na vinywaji kufika hospitalini kuonana na wataalam, kufanyiwa uchungu na kupatiwa matibabu kwa wakati kuepuka madhara makubwa,’’ ameshauri Dk Binde

Ushuhuda wa mgonjwa

Akizungumzia huduma hiyo, Boniface Waryoba, mkazi wa Sengerema aliyepandikizwa koo bandia amewaonda hofu wenye tatizo la maumivu wakati wa kunywa vimiminika na kumeza vyakula kufika hospitalini kwa uchunguzi na tiba akisema haina madhara.

‘’Nimeanza kupata tatizo la maumivu ya koo na kushindwa kunywa wala kumeza chakula tangu mwezi Agosti, mwaka huu; afya na mwili wangu ulianza kudhoofu kwa sababu ya kushindwa kunywa wala kula. Lakini baada ya kuandikiziwa koo bandia sasa naweza kunywa na kula bila shida,’’ amesema Waryoba

Waryoba aliyepandikiziwa koo bandia wiki moja iliyopita anasema hivi sasa hapati maumivu wakati wa kunywa vimiminika na kula chakula kama ilivyokuwa awali kabla ya kupandikiziwa koo bandia.

‘’Sipigi debe, bali nazungumza ushuhuda wa kilichonitokea; nawasihi wenye tatizo la uvimbe, makovu na saratani ya koo wanaoshindwa kumeza chakula wawahi hospitalini kwa uchunguzi na huduma za kiafya kuepuka madhara makubwa,’’ amesema Waryoba