Iran yaigomea Marekani

Muktasari:

Yakataa mazungumzo na nchi hiyo mpaka itakapoondoa vikwazo.

Iran. Serikali ya Iran, imesema kuwa haina mpango wa kufanya mazungumzo na Rais wa Marekani, Donald Trump mpaka pale Taifa hilo litakapoondoa vikwazo dhidi ya nchi yake.

Rais wa Iran, Hassan Rouhani alisema hayo leo Jumatano Septemba 26 kuwa nchi yake haiwezi kufanya mazungumzo wakati ambako Marekeni imeiongezea vikwazo.

Kwa muda mrefu viongozi wa mataifa ya Ulaya wanashinikiza kuwapo kwa mazungumzo baina ya nchi hizo ili kumaliza mgogoro uliopo.

Awali Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron kwa siku mbilimfululizo amekuwa akijaribu kuwakutanisha viongozi hao wawili wakiwa katika mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Rais Macron anajaribu kufanikisha mkutano huo wa kihistoria ambao anatumai utaepusha kutokea vita katika Mashariki Kati.

Hata hivyo, Rais wa Rouhani akihutubia katika Hadhara Kuu ya Umoja wa Mataifa uliofanyika mwishoni mwa wiki alisema hatokubali kufanya mazungumzo wakati Marekani inaendelea kuiwekea vikwazo nchi yake.