Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jaji Mkuu ataka watumishi wa mahakama kurudi darasani

Muktasari:

  • Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma amesisitiza watumishi wa mahakama kote nchini kurudi Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto ili kujifunza mifumo ya kidigitali katika uendeshaji wa shughuli za kimahakama.

Bariadi. Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma amesisitiza watumishi wa mahakama kote nchini kurudi Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto ili kujifunza mifumo ya kidigitali katika uendeshaji wa shughuli za kimahakama.

 Profesa Juma amesema hayo leo Jumatano, Novemba 23, 2022 Mjini Bariadi mkoani Simiyu wakati wa ziara ya Tume ya Mahakama yenye lengo la kukutana na kamati za maadili za wilaya na mkoa, pamoja na wajumbe wa kamati hizo ili kujadili namna ya kuboresha utendaji kazi na kuelewa mipaka ya utendaji kazi.

Ziara aliyoitaja itasaidia tume ya mahakama katika jambo la msingi la maadili katika kutenda haki kwa wananchi.

Amesema kila mtumishi wa mahakama atapata ujuzi wa awali na mafunzo yatahusisha ngazi zote kuanzia madereva, walinzi hadi majaji kwakuwa dunia inahamia kidigitali.

"Tumewekeza kwa kiasi kikubwa katika mifumo ya tehama na kila mtumishi anafahamu umuhimu wa teknolojia katika kuongeza ufanisi, kuweka uwazi na uweledi katika utoaji wa huduma na tumefanikiwa sana," amesema

Profesa Ibrahim amesema dunia ya sasa imefika hatua ambayo inataka kubadilisha utoaji wa huduma kutoka mifumo inayotegemea makaratasi ambayo ni mifumo ya analogia kuingia katika mifumo ya kidigitali na duniani kote uchumi utaenda kwa kasi.

Serikali ya Tanzania tayari imeanzisha mfumo wa nchi wa kidigitali na mahakama haitabaki nyuma kuhakikisha huduma zinapatikana kupitia mfumo wa mtandao na chuo cha uongozi wa mahakama Lushoto kitakamilisha mitaala ya kuwapa ujuzi wa kuwezesha kufanya kazi katika mfumo wa kidigitali.

Katika taarifa iliyotolewa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu ya Shinyanga Athuman Kirati ameelezea kuwa mashauri yote katika mahakama za mkoa wa Simiyu yanafunguliwa kwa kwa njia ya mtandao kwenye JSDSII (Judicial statistical Dashboard System II) na 'Primary Court App.'

Aidha, amesema katika kurejesha imani ya jamii na ushirikishwaji wa wadau katika shughuli za mahakama, kuna utaratibu wa kupokea malalamiko mbalimbali ambayo hufanyiwa na wahusika kupewa mrejesho, wananchi wenye malalamiko husikilizwa kupitia madawati ya malalamiko.

Akitoa muongozo wa malezi kwa kamati za maadili za wilaya na Mkoa Jaji wa mahakama ya rufani, Dk Gerald Ndika amesema mara nyingi malalamiko yao huwa yanatolewa kwa maneno na mengine katika majukwaa hata ya kisasa na vijiwe, andiko ili lishughulikiwe lazima liletwe kwenye kamati husika na liwe kwenye maandishi.

"Asiyejua kusoma ni wajibu malalamiko yake yaandikwe, atie saini au aweke alama ya dole gumba na katibu wa kamati ya mkoa akipokea malalamiko hayo inatakiwa ayawasilishe kwa jaji mfawidhi ili yatolewe maelekezo," amesema Dk Ndika.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Yahya Nawanda amesema elimu walizonazo wataalamu ziakisi kazi wanazozifanya, uwajibikaji na uongozi mzuri unategemea ushauri kutoka kwa wasimamizi na hiyo itasaidia kutengeneza viongozi wazuri.