Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jema: Msiwafiche wenye ulemavu, waleteni wahesabiwe

Mkufunzi wa Sensa ya Watu na Makazi Mkoani Iringa, Jema Mdegela (kushoto) akifanya mazoezi ya kujaza dodoso la majengo alipotembelea nyumba ya Alatanga Maholanga, mkazi wa Ilambilole, Wilayani Iringa

Muktasari:

Tanzania itafanya Sensa ya Watu na Makazi Agosti 23,2022 huku wananchi wakisisitizwa kuwa tayari kuhesabiwa.

Iringa. Mkufunzi wa Sensa ya Watu na Makazi, Jema Mdegela ameiomba jamii kutokubali mila na desturi zinazowaficha watu wenye ulemavu ili wasihesabiwe kwenye shughuli ya sensa ya watu na makazi Agosti 23, 2022.

Jema amesema hayo jana Jumapili Julai 22, 2022 wakati akizungumza na Alatanga Maholela, mlemavu wa viungo na mkakazi wa kijiji cha Ilambilole wakati timu ya wakufunzi ilipotembelea eneo hilo kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo kwenye dodoso la majengo.

Amesema watu wenye ulemavu wanayo haki ya kuhesabiwa na kusikilizwa changamoto zao.

“Namie mwenyewe nashukuru kupata nafasi hii, niliteuliwa nikiwawakilisha watu wenye ulemavu wenzangu, hii inaonyesha Serikali yetu inajali makundi maalu,” amesema Jema, mdogo wa msanii maarufu nchini, Tausi Mdegela.

Awali, Mratibu wa Sensa ya Watu na Makazi Mkoani Iringa, Peter Milinga amesema hakuna mila na desturi finyu iliyojitokeza kukwamisha sensa itakayofanyika Agost 23, 2022.

Amesema tayari wameanza kupokea vifaa mbalimbali ikiwamo vishikwambi zaidi ya 4600 kwa ajili ya maandalizi.

Milinga amesema hayo wakati timu ya wakufunzi wa makarani wa sensa walipokuwa wakifanya mazoezi ya vitendo kwenye dodoso la majengo, katika kijiji cha Ilambilole, Wilayani Iringa.

“Tupo kwenye hatua nzuri, mpaka sasa hakuna kitu kilichotukwamisha na hawa wanaofanya mazoezi ni walimu wa makarani ambao moja kwa moja wanaenda kufanya kazi wenyewe,” amesema Milinga na kuongeza:

“Bado sijakutana na tatizo la mila wala tamaduni zinazokataza kuhesabiwa na niendelee kuwakumbusha wana Iringa kwamba suala na sensa ni la Baraka.”

Awali, akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Queen Sendiga, Mkuu wa Wilaya ya Kilolo, Saad Mtambule aliwaka wakazi wa mkoa huo kuachana na mila finyi zenye lengo la kukwamisha zoezi hilo

“Tupo vizuri na maandalizi ni mazuri mpaka sasa,” alisema Mtambule.