Jokate Katibu Mkuu mpya UWT

Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imemteua Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga, Jokate Mwegelo kuwa Katibu Mkuu ya Umoja wa Wanawake (UWT).
Kabla ya uteuzi huo wa Jokate, nafasi ya Katibu Mkuu wa UWT ilikuwa ikishiliwa na Dk Phillis Nyimbi.
Mbali na Jokate, pia CCM imemteua Mkuu wa Wilaya ya Momba mkoani Songwe, Fakii Raphael Lulandala kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana (UVCCM). Awali, nafasi hiyo ilikuwa wazi baada ya Kenani Kihongosi kuteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Iramba mkoani Singida.