Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jokate, Lulandala wateuliwa CCM

Muktasari:

  • Chama cha Mapinduzi (CCM) kimemteuwa Jokate Mwegelo kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake wa chama hicho (UWT).

Dar es Salaam. Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM imemteuwa, Jokate Mwegelo kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT).

Pamoja naye, Raphael Lulandala ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM).

Kulingana na taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Katibu wa NEC ya CCM, Itikadi na Uenezi, Sophia Mjema, wawili hao kabla ya kuteuliwa katika nafasi hizo walikuwa Wakuu wa Wilaya, Jokate akiwa, Korogwe mkoani Tanga, huku Lulandala akiwa Momba mkoani Songwe.

Kutokana na uteuzi huo, Jokate anamrithi Dk Philis Nyimbi na Lulandala anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Kenani Kihongosi aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Urambo Mei 23, mwaka huu.


Jokate ndani, nje ya CCM

Safari ya Jokate katika Chama Cha Mapinduzi (CCM) ilianza mwaka 2017, alipoteuliwa kuwa Katibu wa Idara ya Uhamasishaji ya Umoja wa Vijana ya chama hicho (UVCCM).

Baadaye mwaka 2018, Rais wa awamu ya tano, John Magufuli alimteuwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani na baadaye alihamishiwa Temeke jijini Dar es Salaam, kabla ya kupelekwa Korogwe mkoani Tanga kwa wadhifa huo.

Nje ya CCM, Jokate aliwahi kushika nafasi ya pili katika mashindano ya ulimbwende mwaka 2006 na baadaye akashiriki shughuli za sanaa ya muziki na uigizaji.


Lulandala

Kwa upande wa Lulandala, safari yake ya siasa imehusisha chama cha Chadema ambapo mwaka 2015 alikuwa Mwenyekiti wa chama hicho mkoani Njombe.

Kipindi hicho hicho, Lulandala aliwania ubunge wa Njombe Kusini kupitia Chadema na Agosti 12, 2018 alijiuzulu nafasi hiyo na kujiunga na CCM.