Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

JPM: Mwalimu mkuu atakayeruhusu aliyepata mimba kurudi shule ataondoka

Rais John Magufuli

Muktasari:

  • Rais Magufuli amesisitiza kuwa mwalimu mkuu yeyote atakayefanya ujanja wa kumrudisha mtoto aliyepata mimba, mwalimu huyo ataondoka.

Sengerema. Rais John Magufuli amesema mwalimu mkuu atakayeruhusu mwanafunzi aliyejifungua kurudi shuleni kuendelea na masomo katika shule za Serikali, atafukuzwa kazi.

Rais ameyasema hayo leo (Jumanne, Julai 4) alipokuwa akihutubia wananchi wakati akizindua mradi wa maji Sengerema.

“Ni ukweli pia kuwa wanafunzi waliopata mimba hawarudishwi shuleni, kuna ujanja ujanja wa walimu, wanaandika cheti kuwa alikuwa amelazwa,” amesema na kuongeza:

“Nikimuona Headmaster, amerudisha mwanafunzi aliyepata mimba, kwenye shule za Serikali, yule mwalimu anaondoka.”

Rais amehoji: “Wote waliopata mimba wamebakwa?” Alihoji na kuendelea, “wanafanya mambo haya kwenye picha, wakipata mimba kwa namna hiyo arudi shule.”

Ameongeza: “Niwaombe wazazi wawachunge watoto, hizi mimba zinatokana na wazazi wetu ni lazima wazazi tujifunze kulea, tumechagua kueleza ukweli, tuambiane ukweli.”