Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kaburi la Ruge laandaliwa, viongozi waendelea kumlilia

Muktasari:

  • Jana, Mwananchi ilishuhudia shughuli za uchimbaji kaburi na maandalizi mengine yakiendelea kijijini hapo.

Bukoba. Unaweza kusema safari ya Ruge Mutahaba hapa duniani imebakiza saa chache tu. Jumatatu Machi 3, mwili wake utalazwa katika nyumba yake ya milele iliyoanza kuandaliwa kijijini kwao Kiziru, Bukoba mkoani Kagera.

Familia yake iliyopo kijijini hapo, jana ilianza kumuandalia nyumba hiyo pembezoni mwa makaburi mengine ya wanafamilia wengine waliotangulia mbele za haki.

Kaburi la Ruge, mtu aliyejitoa maisha yake kuinua burudani, kuendeleza vijana, kusaidia kutatua matatizo na kuvumbua akili wajasiriamali, ni la 10 katika eneo hilo na baadhi ya waliozikwa ni babu yake Mzee Mbeikya, Koburungo Mbeikya (Bibi), Jafary Rwabyo (babu mdogo), Fatuma Mbeikya (dada wa babu) na Joyce Mbeikya (shangazi yake).

Viongozi mbalimbali na wanausalama walifika kijijini hapo kukagua na kufanya maandalizi mengine ya mapokezi ya ugeni mkubwa unaotarajia kufika kwa ajili ya shughuli hiyo ya kumzika.

Kijiji hicho kipo Kata ya Karabagaine na Mwananchi ilishuhudia askari wa usalama barabarani wakikagua barabara itakayotumika kupita msafara wenye jeneza.

Mwili wa Ruge unatarajiwa kuwasili uwanja wa ndege wa Bukoba Jumapili na maziko kufanyika Machi 3 na baadhi ya wageni wameanza kuwasili.

Speratus Mbeikya, baba mdogo wa Ruge, alisema uchimbaji wa kaburi na ujengaji wake unaendelea na baadhi ya vijana walikuwa wakiendelea na kazi hiyo.

Mbeikya alisema wameanza kupokea wageni kutoka maeneo mbalimbali na tayari wamekubaliana na askari wa usalama barabarani maeneo utakapopita msafara wenye mwili wa marehemu.

Alisema kwa kifupi Ruge-- kirefu ni Rugemarila--ni linalomaanisha mtu jasiri na mpambanaji.

Naye binamu yake, Angelina Paschal alimtaja Ruge kama ndugu aliyekuwa msaada mkubwa kwao na mara nyingi alikuwa akiwasisitizia umuhimu wa binadamu kusaidiana.

Alisema ndiye alikuwa anampikia chakula kila alipofika nyumbani hapo kwa mapumziko na mara ya mwisho alifanya hivyo mwaka 2017 alipofika kwa ajili ya kusherehekea sikukuu za mwisho wa mwaka.

Kikwete amlilia

Jijini Dar es Salaam, Rais Jakaya Kikwete aliyefika kutoa salamu za pole kwa familia ya Ruge jana, Mikocheni, alisema nchi imepoteza mzalendo wa kweli.

Kikwete alisema Ruge, tofauti na vijana wengine, alikuwa akifanya mambo kwa ajili ya wengine.

“Ukimfuatilia sana kuhusu kazi zake, utagundua wakati alikuwa anafanya anashughulika kwa sababu ya wenzake. Angalia Fursa (semina za uhamasishaji ujasiriamali), Vijana Think Tank na mengine mengi, hakufanya haya kujinufaisha, aliishi vizuri kwa hiyo sisi tujitahidi kufuata mfano wake,” alisema Kikwete.