Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kaburi la Ruge Mutahaba laanza kuchimbwa

Muktasari:

Uchimbaji wa kaburi atakalozikwa Ruge Mutahaba umeanza leo kijijini kwao Kiziru wilaya ya Bukoba mkoa wa Kagera.


Bukoba.  Maandalizi ya kumzika marehemu Ruge Mutahaba katika Kijiji cha Kiziru, Wilaya ya Bukoba Mkoa wa Kagera yanaendelea na hivi sasa uchimbaji wa kaburi umeanza rasmi leo Alhamisi Februari 28,2019.

Akizungumzia maandalizi hayo Siperatus Mbeikya,  mmoja wa wanafamilia aliyeko Bukoba amesema taratibu zinaendelea ikiwa ni pamoja na kupokea wageni kutoka maeneo mbalimbali.

Pia, amesema maandalizi hayo yamekwenda sambamba na kukubaliana na kikosi cha usalama barabarani  sehemu utakapopita msafara wenye mwili wa marehemu Ruge aliyefariki juzi Jumanne nchini Afrika Kusini alipokuwa akipatiwa matibabu tangu mwaka jana.

Pilikapilika zimeongezeka katika eneo la msiba ikiwa ni pamoja na kumwaga vifusi kwenye maeneo ya barabara yaliyo korofi

Nyumbani kwa kina Ruge katika kijiji hicho baadhi ya ndugu wa karibu walikuwa wakiendelea na kikao cha maandalizi ya msiba huo ambapo marehemu Ruge anatarajiwa kuzikwa siku ya Jumatatu, Machi 3.