Kada wa CCM atiwa ngeu kichwani kisa wivu wa mapenzi

Muktasari:

  •  Ni mshangao, ndivyo unavyoweza kueleza mkasa uliompata mmoja wa viongozi wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) wilayani Chemba Mkoa wa Dodoma, kupigwa na kitu chenye ncha kali kichwani  na kiongozi wa Umoja wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) katika mgogoro unaodaiwa kuwa wa mapenzi.


Dodoma. Ni mshangao, ndivyo unavyoweza kueleza mkasa uliompata mmoja wa viongozi wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) wilayani Chemba Mkoa wa Dodoma, kupigwa na kitu chenye ncha kali kichwani  na kiongozi wa Umoja wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) katika mgogoro unaodaiwa kuwa wa mapenzi.

Tukio hilo lilitokea mwisho wa wiki iliyopita, muda mfupi baada ya wajumbe kumaliza uchaguzi wa Katibu Mwenezi wa wilaya wa chama hicho.

Tangu juzi zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) wa wilaya kupasuliwa ngeu na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT) wa wilaya hiyo.

Taarifa hiyo, imesema kuwa kiongozi wa kiongozi huyo wa UWT kumfuata kiongozi mwenzake katika kibanda cha Mama lishe na kisha kumpiga kwa kutumia jagi la kioo ambalo lilimpasua sehemu kubwa ya kichwa.

Katibu wa CCM wilaya ya Chemba, Himid Tweve jana amethibitisha kuwepo kwa tukio hilo lakini akasema ni mapema kulizungumza kwani vyombo vingine ikiwemo vya chama vinalifanyia kazi.

“Ni kweli tukio hilo lipo, hata sisi tulisikia kama mnavyosikia ninyi lakini tumeshuhudia katibu wetu amepigwa, isipokuwa siwezi kusema zaidi kwa kuwa chama chetu kina maadili na miiko yake utafika wakati ambao tutasema,” alisema Tweve.

Hata alipotakiwa kuzungumzia mienendo ya Mwenyekiti huyo ambaye ni mjumbe wa Kamati ya siasa ya wilaya na Katibu ambaye ni Mjumbe wa Sekretarieti, aligoma kwamba mambo kama hayo yanahusu watu wawili.

Mmoja wa wajumbe wa halmashauri ya wilaya ameeleza namna tukio hilo lilivyokuwa kwamba kiongozi wa UWT alimfuata mwenzake katika mgahawa alipokuwa anakula chakula na kupiga kwa jagi la kioo kichwa.

Shuhuda huyo ambaye ni diwani wa viti maalumu, alisema wakati wote wawili hao wamekuwa na mzozo wa chinichini kutokana na mahusiano yao kuwa yameingiliwa na mtu mwingine ambako jana majeruhi huyo alikutwa akila chakula.

 “Tulikuwa na uchaguzi wa Katibu wa Itikadi,Siasa na Uenezi wa wilaya na tulipomaliza ndipo Kiula alikwenda katika mgahawa huo kwa ajili ya chakula cha mchana akiwa peke yake,” alisema mtoa taarifa.

Taarifa zinaeleza kuwa alipokwenda Kiula ni mgahawa wa mwanamke mmoja ambaye amekuwa akitiliwa shaka na kiongozi huyo wa UWT anayedaiw akuwa na uhusiano naye kimapenzi.

Taarifa hizo zinasema kuwa, kiongozi huyo wa UVCCM alifuatwa na kabla ya kupigwa ngeu, aliulizwa ni kwa nini alikwenda mahali ambapo amekuwa akizuiwa kutofika.