Kamanda wa Polisi Kinondoni aanza kutoa ushahidi kesi ya Mbowe

Kamanda wa Polisi Kinondoni aanza kutoa ushahidi kesi ya Mbowe

Muktasari:

  • Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi imeanza kupokea ushahidi kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Ramadhani Kingai katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu.

Dar es Salaam. Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi imeanza kupokea ushahidi kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Ramadhani Kingai katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu.


Kamanda wa polisi ni miongoni mwa mashahidi katika keshi hiyo, mashahidi wengine ni pamoja na aliyekuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Boaz.


Wengine ni maofisa wa polisi kutoka makao makuu ya jeshi hilo vitengo vya makosa ya kimtandao, uchunguzi wa silaha na uchunguzi wa maandishi na wengine kutoka mikoani.


Mashahidi wengine ni maaskari kutoka Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), akiwamo Luteni Denis Leo Urio kutoka Kikosi cha Jeshi cha Makomandoo, 92 KJ Ngerengere, mkoani Morogoro.

Soma zaidi: Boaz, Kingai kizimbani kesi ya Mbowe
Pia wamo maofisa wa sheria kutoka kampuni za huduma za simu za mkononi za Mic Tanzania Ltd (Tigo) na Aritel.