Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kamishna Jenerali afichua mbinu wanawake wanavyotumika kusafirisha dawa za kulevya

Kamishna Jenerali Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya, Aretas Lyimo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam. Picha na Michael Matemanga

Muktasari:

  • Mzigo mkubwa wa dawa za kulevya wakamatwa ndani ya miezi mitatu, wanawake watahadharishwa kutumika kusafirisha dawa hizo.

Dar es Salaam. Jumla ya kilogramu 200.5 ya dawa za kulevya aina ya heroine, cocaine kete 138 na metamphetamine gramu 532.1 zimekamatwa katika kipindi cha miezi mitatu.

Mbali na dawa hizo zimekamatwaa pia kilo 1.5 ya bangi iliyosindikwa, magunia 978 ya bangi kavu, magunia 5,465 ya bangi mbichi na ekari 1,093 ya mashamba ya bangi.

Hayo yamebainika katika taarifa ya Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.

Kamishna Jenerali Lyimo ameeleza kuwa ukamataji huo ulifanyika kati ya Machi 25 hadi Juni 19 katika mikoa ya Dar, Pwani, Arusha na Kilimanjaro umeweza kuwanasa watuhumiwa 109 wakiwemo raia watatu wa kigeni.

Kamishna pia ametahadharisha uwepo wa mbinu mpya ya wafanyabiashara wa dawa za kulevya kuwatumia wanawake kusafirisha dawa hizo hali inayowaweka matatani.

“Kutokana na udhibiti mkubwa wafanyabiashara hawa wamebuni mbinu mpya hasa raia wa kigeni kuanzisha uhusiano wa kimapenzi na wanawake wa Kitanzania.

“Niwatahadharishe wanawake wasikubali kuanzisha uhusiano na watu wasiowafahamu, huwa wanawatumia kusafirisha dawa za kulevya au kuzihifadhi kwenye nyumba zao. Tunapowakamata mzigo unakutwa kwa mwanamke na yule mwanaume anamkana kabisa,”amesema Kamishna Jenerali Lyimo.