Kampeni ya chanjo ya Uviko- 19 kufanyika kwa wavuvi Buchosa

Muktasari:

  • Jamii ya wavuvi imeshukuru vyombo vya habari kujikita maeneo yao kuisemea changamoto zao na Serikali umeamua kufika kwao lengo la kutoa elimu na chanjo ya Uviko 19.

Buchosa. Kutokana na mahitaji ya chanjo ya Uviko 19 kwa wavuvi waliopo kwenye visiwa vilivyoko Buchosa wilayani Sengerema Mkoa Mwanza, timu ya afya inaanza kampeni ya kutoa elimu pamoja na chanjo ya Uviko 19 Septemba 20 mwaka kwa jamiii hiyo.

Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Buchosa Wilayani Sengerema mkoa Mwanza, Dk Irene Mukerebe ameliambia Mwananchi leo Septemba 19 kuwa timu hiyoitazunguka visiwa hivyo na kutoa chanjo ya Uviko 19 kwa wavuvi.

Amsema kampeni hiyo itaanzia kisiwa cha Maisome kwenye kambi za uvuvi na maeneo mengine kwa lengo la watu kupata chanjo ya Uviko 19 Ili kujikinga na ugonjwa huo.

"Tunaomba watu wajitokeze kwa wingi kupata elimu Kisha chanjo ya Uviko 19 ambayo inatolewa bure kote nchi," amesema Dk Mukerebe.

Kwa upande wake ofisa Mtendaji Kata ya Maisome, Onesmo Daudi amesema wamejipanga kutoa matangazo Kila mahali ili Wananchi wajitokeze kupata elimu na chanjo hiyo.

"Imani yangu kubwa watu watajitokeza na kupata chanjo ya Uviko 19 kutokana na hamasa tutakayofanya " amesema Daudi.

Kisiwa cha Maisome nimuunganiko wa Visiwa vya Rubaragazi kubwa, Rubarazi ndogo, vijiji vya Busikimbi, Kanoni pamoja na Kisaba.

Mmoja wa wakazi wa Kijiji cha Kisaba kisiwa cha Maisome Anastazia Faustine amesema kama timu hiyo ya afya itafika kwenye Visiwa na kutoa hamasa Wananchi wengi watajitokeza kupata chanjo hiyo.