Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kampuni binafsi za ulinzi zabainika kumiliki silaha kinyemela

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Janeth Magomi akionyesha moja ya silaha zilizokamatwa zikimilikiwa kinyume cha sheria na kampuni binafsi za ulinzi wilayani Kahama. Picha na Suzy Butondo.

Muktasari:

Kampuni binafsi tano za ulinzi Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga zimebainika kumiliki bunduki na risasi kinyume cha sheria.

Shinyanga. Kampuni tano binafsi za ulinzi Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga zimebainika kumiliki bunduki na risasi kinyume cha sheria.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Janeth Magomi amewaambia waandishi wa habari leo Alhamisi Aprili 27, 2023 kuwa Jeshi la Polisi limebaini uhalifu huo baada ya kufanya operesheni maalum ya kushtukiza katika maeneo ya  Shunu, Nyihogo, Malunga, Mhongolo, na Nyasubi wilayani Kahama.

“Oparesheni hiyo ya polisi ilifanyika kwa kufanya ukaguzi wa kushtukiza katika maeneo ya lindo ya makampuni binafsi ya ulinzi katika Wilaya ya Kahama ambapo makampuni hayo yamekutwa yakimiliki bunduki tano kinyume cha kifungu 10 (7) cha sheria ya usimamizi na udhibiti wa silaha na risasi ya mwaka 2015,” amesema Kamanda Magomi.

Ametaja bunduki zilizokutwa zikimilikiwa kinyume cha sheria na makampuni hayo kuwa ni aina ya Mark IV iliyokutwa na risasi nne, Mark IV iliyokutwa na risasi tatu, Mark IV iliyokutwa na risasi moja, Mark IV iliyokuwa na mbili na Short Gun iliyokutwa na risasi moja.

Katika hatua nyingine, Kamanda Magoma amesema Jeshi hilo limefanikiwa kunasa mali kadhaa zinazoaminika kuwa za wizi ikiwemo magodoro, simu za kiganjani, kompyuta, mitungi ya gesi, Runinga na pikipiki sita.

Jeshi hilo limefanikiwa kuwatia mbaroni watuhumiwa 132 kwa makosa mbalimba yakiwemo ulawiti, ukatili na unyanyasaji kijinsia, mimba kwa wanafunzi na ubakaji.