Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kikaratasi cha mtoto mgonjwa chamfikia Majaliwa, ampa maagizo Dk Mollel

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimuagiza Naibu Waziri wa Afya Dk. Godiwn Mollel kumsaidia mtoto Zahir wa Kijiji cha Nanguruwe Halmashauri ya Wialaya ya Mtwara anayesumbuliwa na tatizo la moyo. Picha na Florence Sanawa

Muktasari:

  • Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameendelea na ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ambapo amemuagiza Naibu Waziri wa Afya, Dk Godwin Mollel kumsaidia mtoto Zahir wa kijiji cha Nanguruwe ili apatiwe matibabu ya moyo.

Mtwara. Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa ametoa maagizo kwa Naibu Waziri wa Afya, Dk Godiwn Mollel kumsaidia mtoto Zahir wa kijiji cha Nanguruwe ili apatiwe matibabu ya moyo.

Baada ya mama yake kuandika karatasi na kuomba msaada wa matibabu kwa Serikali kutokana na kushindwa kumudu gharama za matibabu hayo zaidi ya Sh28 milioni. 

Majaliwa akiwa katika ziara yake alisimama katika kijiji cha Nanguruwe ambapo alipokea karatasi yenye ujumbe wa maandishi ya kuomba msaada wa matibabu kutoka kwa mama wa Zahir, Aisha Luyenda aliyekuwepo barabarani hapo.

Alisema mtoto huyo alibainika kuwa na tatizo la moyo kuelekea upande wa kulia wa kifua badala ya kushoto (Dextrocardia) na kwamba anahitaji matibabu makubwa zaidi lakini hana uwezo wa kumpa matibabu mtoto huyo.

Kwa mujibu wa Waziri Mkuu kupitia maandishi hayo alisema mama huyo ameeleza tiba ya moyo kama hiyo inagharimu Sh28 milioni ambapo mama huyo ameeleza hana uwezo na kuomba msaada kwa serikali.

Akipokea maagizo hayo, Dk Mollel naye alimuagiza Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Hamad Nyembea kusimamia maandalizi ya mtoto Zahir ili aweze kufika katika Taasisi ya Jakaya Kikwete (JKCI) jijini Dar es Salaam na siku ya Jumatatu ili afanyiwe uchunguzi zaidi.

“Mara nyingi unaweza kuambiwa kuwa moyo uko huku moyo uko kule anaweza kuwa na tundu kwenye moyo ama tatizo alilozaliwa nalo kwenye moyo zipo fedha ambazo Serikali imetenga kwaajili ya kuweza kuwasaidia watoto wenye matatizo kama ya huyu ambao wazazi wao hawana uwezo” alisema Dr Mollel

“Namwaagiza Mganga Mkuu wa Wilaya abaki amuangalie huyu mtoto, Mganga Mkuu wa Mkoa atoe gari na Mganga wa Hospitali ya mkoa atoe mafuta mtoto afike Dar es Salaam apokelewe ili Jumatatu aanze matibabu haraka,” alisema Dkt Mollel