Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kilo 276 za dawa za kulevya zakamatwa Iringa

Muktasari:

  • Kilo 276 za dawa za kulevya zakamatwa Iringa katika operesheni ya kutokomeza mtandao wa biashara ya dawa hizo haramu.

Iringa. Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama, imefanya  operesheni maalum katika Mkoa wa Iringa na kufanikiwa kukamata jumla ya kilo 276 za dawa za kulevya aina  heroin na bangi.

Operesheni hiyo imewezesha pia kuwakamata watu 12 wanaotuhumiwa kuhusika na dawa hizo.

Taarifa iliyotolewa leo Jumapili Agosti 27 na Ofisa Mawasiliano Mwandamizi,  Daniel Kasokola kwa niaba ya Kamisha Jenerali wa mamlaka hiyo imeeleza kuwa operesheni hiyo inalenga kutokomeza mitandao ya biashara ya dawa za kulevya.

Amesema Serikali kuwa imejipanga kikamilifu kukabiliana na dawa za kulevya nchini, hivyo kwa sasa Tanzania siyo sehemu salama kwa wote wanaojihusisha na biashara au kilimo cha dawa za kulevya.

“Operesheni hizi ni moja ya utekelezaji wa mkakati  wa kudhibiti upatikanaji wa dawa za kulevya hivyo kama Kamishna Jenerali anavyoeleza operesheni hizi zitafanyika nchi zima, tuhakikishie tutawakamata vinara wote  wanaojihusisha na kilimo au biashara ya dawa za kulevya kwani mitandao yao na mbinu zao tunazijua hivyo hakuna mhalifu wa dawa za kulevya ambaye ataukwepa mkono wa sheria.

“Niwaombe Watanzania wenzangu waungane na Serikali katika mapambano  haya kama walivyofanya wananchi wa Kisimiri juu, Lesinoni na Lenglong  mkoani Arusha na wananchi wa walaya ya Same mkoani Kilimanjaro kuamua  kwa hiari yao kuondoa mimea ya bangi na mirungi katika maeneo yao,”amesema Kasokola.

Akizungumzia operesheni hiyo Mtendaji wa kata ya Malolo wilaya ya Kilosa, Fredinand Litweka amesema kufanyika kwa operesheni hiyo kutasaidia kupunguza kilimo cha bangi katika eneo hilo kutokana na kuanza kushamiri kwa mashamba ya zao hilo.

“Mashamba ya bangi yameshamiri, uongozi wa wilaya umekuwa wakifanya jitihada kadhaa bila mafanikio hivyo, kufika kwa mamlaka katika maeneo yetu kutaongeza chachu ya mapambano dhidi ya kilimo na biashara ya dawa za kulevya,” amesema Litweka.