Kisena wa Udart, wenzake wafikishwa mahakamani

Wednesday July 06 2022
udartpiic
By Hadija Jumanne

Dar es Salaam. Mkurugenzi wa mradi wa Usafirishaji wa Mabasi yaendayo Haraka Dar es Salaam, (Udart) Robert Kisena(47) na wenzake wawili, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka 25 yakiwemo ya wizi, kutakatisha fedha, kuisabaishia Serikali hasara  ya Sh4.4bilioni pamoja na kuongoza genge la uhalifu.

Washtakiwa hao wamesomewa mashtaka yao leo Jumatano Julai 6, 2022 na wakili wa Serikali, Timotheo Mmari akisaidiana na Aboud Yusuph, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi.

Mbali na Kisena washtakiwa wengine katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 40 ni Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Simon Group Ltd, Charles Newe(48) na mfanyabiashara Kulwa Kisena(34).

Advertisement