Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kiwanda cha Wachina Dodoma chafungiwa

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Walemavu, Antony Mavunde

Muktasari:

Mavunde amechukua uamuzi huo katika kiwanda hicho kilichopo Zuzu nje ya Mji wa Dodoma, baada ya kukitembelea na kushuhudia mambo mbalimbali yanayofanyika kinyume cha sheria, huku ikiwa na idadi kubwa ya wageni ambao wanafanya kazi bila ya vibali.

Dodoma. Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Walemavu, Antony Mavunde amekifunga kwa muda kiwanda cha kutengeneza mbao nyepesi cha S & Y Company Ltd na kuwatoza wamiliki faini ya papo hapo ya Sh4 milioni na kuwataka raia 10 wenye asili ya China kujisalimisha Uhamiaji.

Mavunde amechukua uamuzi huo katika kiwanda hicho kilichopo Zuzu nje ya Mji wa Dodoma, baada ya kukitembelea na kushuhudia mambo mbalimbali yanayofanyika kinyume cha sheria, huku ikiwa na idadi kubwa ya wageni ambao wanafanya kazi bila ya vibali.

Kiwanda hicho kinachotegengeza mbao, upande wa pili kinatumika kwa machinjio ya nyama, lakini kiko katika mazingira machafu.

Hata hivyo, kiongozi huyo alikutana na ugumu mlangoni kwani licha ya kujitambulisha, hakuruhusiwa kuingia hadi msaidizi wake alipoamua kutumia nguvu kufungua geti.

Raia hao walipobaini ameingia, waliwasha magari na kuanza kukimbia kabla ya kuzuiwa getini na wasaidizi waziri.

Kiwanda hicho kina wafanyakazi zaidi ya 80 Watanzania na raia 10 wa China, lakini mazingira yake ni hatarishi kwa afya zao na hakuna mfanyakazi aliyeonekana kuwa na vifaa vya usalama.

“Nimechukizwa na hiki nilichokiona hapa, kwanza sikutegemea kukutana na vitu hivi, Watanzania wanaishi maisha kama watumwa kwa sababu gani? Hapafai hapa kwa wakati huu lazima nifunge hadi mtakapojirekebisha,” amesema Mavunde.

Meneja Msaidizi wa kiwanda hicho, Titus Gembe amesema kilianza uzalishaji Novemba, mwaka jana, huku akikiri kwa waziri kuwa hakuna mfanyakazi aliyepewa vifaa vya kazi na wote hawana mikataba licha ya kuwa mazingira ya hapo ni hatarishi.

Alipoulizwa ni kwa nini watu wanafanya kazi kwenye mashine kubwa lakini hawana hata kandambili za kuvaa, meneja huyo alimuomba radhi naibu waziri akimsihi asikifunge kiwanda hicho.

Mtendaji Mkuu wa kiwanda hicho aliyejitambulisha kwa jina la Su, amekiri kuwa na upungufu katika kiwanda chake kwa mujibu wa sheria za kazi, lakini akasema atarekebisha.