Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kuanzia Machi mosi Wasafi TV ruksa kurusha matangazo

Kuanzia Februari 28 Wasafi TV ruksa kurusha matangazo

Muktasari:

  • Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeipunguzia adhabu televisheni ya Wasafi TV kutoka kifungo cha miezi sita na kuiruhusu kuendelea kurusha matangazo yake kuanzia Machi mosi.

Dar es Salaam. Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeipunguzia adhabu televisheni ya Wasafi TV kutoka kifungo cha miezi sita na kuiruhusu kuendelea kurusha matangazo yake kuanzia Machi mosi.

Januari 5, 2021 TCRA ilitoa uamuzi wa kuifungia televisheni hiyo kwa kipindi cha miezi sita kutokana na kukiuka kanuni za mawasiliano ya kielektroniki na Posta.

Taarifa iliyotolewa leo Alhamisi Februari 4, 2021 na mkurugenzi mkuu wa TCRA, James Kilaba imetaja masharti matatu kwa televisheni hiyo ikiwemo  kuendelea kutumikia kifungo hicho mpaka tarehe tajwa.

“Wasafi TV itaendelea kutumikia adhabu hiyo mpaka Februari 28, 2021 pia inaelekezwa kuzingatia masharti ya leseni ya kutoa huduma za maudhui ya kulipia kwa njia ya televisheni na iwapo itashindwa, itakataa au kukaidi uamuzi huu hatua zaidi za kisheria na kiudhibiti zitachukuliwa dhidi ya yake,” ameeleza.

Kilaba amesema kufuatia uamuzi wa kuifungia, Januari 21, 2021 Wasafi iliwasilisha maombi TCRA na vielelezo zaidi ikiomba kupitia upya uamuzi wake na Januari 28,  2021  ilifika tena kwa ajili ya kusikilizwa maombi hayo.

Amesema Wasafi iliwasilisha ushahidi mpya kuonyesha kuwa endapo ushahidi huo ungewasilishwa awali wakati wa usikilizwaji, TCRA isingetoa  adhabu ya kuifungia miezi sita.

Amebainisha kuwa televisheni hiyo ilikiri kurusha matangazo mubashara kinyume na masharti ya leseni yao, na iliomba TCRA kupitia upya uamuzi wake na kuwapunguza adhabu.

“Baada ya kusikiliza wasilisho la Wasafi,  TCRA imetafakari upya uamuzi wake wa Januari 5,  2021 kwa kuzingatia ushahidi uliowasilishwa pamoja na hatua zilizochukuliwa na Wasafi baada ya kosa kutendeka na hivyo basi TCRA imepunguza adhabu hiyo,” amesema Kilaba.