Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Likizo ya Hakimu yakwamisha kesi ya DED na wenzake 10 Kigoma

Muktasari:

Pamoja shtaka la kutakatisha fedha, wanashtakiwa hao pia wameshtakiwa kwa makosa ya kula njama kwa nia ya kutenda kosa, kugushi nyaraka, matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia Serikali hasara ya sh463.5.

Kigoma. Likizo ya Hakimu mkazi mfawidhi Mahakama ya Wilaya ya Kigoma, Hassan Momba imesababisha kuahirishwa kwa shauri la jinai namba 3/2023 linalowakabiliwa washtakiwa 11 akiwemo Mkurugenzi mtendaji wa zamani wa Manispaa ya Kigoma Ujiji, Athumani Msabila.

Pamoja na mashataka mengine, Msabila ambaye hadi anakamatwa na kushtakiwa alikuwa Mkurugenzi mtendaji Halmashauri ya Igunga na wenzake wanadaiwa kufanya kosa la kutakatisha Sh463.5 milioni.

Akiahirisha shauri hilo leo Desemba 4, 2023, Hakimu mkazi Mwandamizi Mahakama ya Wilaya ya Kigoma, Eva Mushi amesema kesi hiyo sasa itatajwa tena Desemba 18, 2023.

‘’Shauri hili linaahirishwa hadi Desemba 18, 2023, muda ambao Hakimu Momba atakuwa amerejea kutoka likizo,’’ amesema Hakimu Mushi

Awali, upande wa Mashtaka kupitia kwa Wakili wa Serikali, Antia Julias aliiambia Mahakama kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika na kuomba tarehe nyingine kwa ajili ya kesi hiyo kutajwa.

Kutokana na taarifa hiyo ya upande wa mashtaka, Wakili wa utetezi, Michael Mwangati ameiomba Mahakama kuuagiza upande wa Jamhuri kuharakisha upelelezi kuwezesha shauri hilo kusikilizwa na kuamuliwa ili kutenda haki kwa pande zote zinazohusika.

Hadi sasa, washtakiwa watano kati ya 11 wanaokabiliwa na kesi hiyo wameahiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti huku wengine sita wakiendelea kusota mahabusu.

Wliotimiza masharti ya dhamana ni pamoja na Joel Shirima, Jema Mbilinyi, Kombe Kabichi, Frank Nguvumali na Bayaga Ntamasambilo.

Wanaoendelea kusota mahabusu tangu Novemba 7, 2023 shauri hilo lilipofikishwa mahakamani ni pamoja na aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Igunga, Athumani Msabila, Aidan Mponzi, Tumsifu Kachira, Frednand Filimbi, Salum Juma na Moses Zahuye.

Washtakiwa katika shauri hilo walikuwa ni watumishi wa umma kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma na Tamisemi.

Pamoja shtaka la kutakatisha fedha, wanashtakiwa hao pia wameshtakiwa kwa makosa ya kula njama kwa nia ya kutenda kosa, kugushi nyaraka, matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia Serikali hasara ya sh463.5.