Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

LIVE: Rais Samia akifungua kikao kazi maafisa waandamizi Jeshi la Polisi

🔴#𝐋𝐈𝐕𝐄: RAIS SAMIA AKIFUNGUA KIKAO KAZI CHA MAAFISA WAANDAMIZI WA JESHI LA POLISI MAKAO MAKUU

Muktasari:

  • Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewasili katika ukumbi wa shule ya polisi Tanzania(TPS) Mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya ufunguzi kikao kazi cha Maofisa wakuu waandamizi wa polisi wa makao makuu, Makanda wa polisi wa mikoa na vikosi.



Moshi.  Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewasili katika ukumbi wa Shule ya Polisi Tanzania(TPS) mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya ufunguzi kikao kazi cha Maofisa wakuu waandamizi wa polisi wa makao makuu, makamanda wa polisi wa mikoa na vikosi.

Kikao hicho ambacho ni cha siku tatu kinaanza leo Agosti 30 hadi Septemba Mosi, 2022 ikiwa ni utaratibu wa Jeshi la polisi kila mwaka kufanya kikao kwa lengo la kufanya tathmini ya utendaji katika kipindi cha mwaka mmoja.

Katika kikao hicho wataangalia walipofanya vizuri na wapi ambapo hawakufanya vizuri na sababu zake ili kuweka mikakati mipya ya kutekeleza majukumu ya jeshi hilo kwa ufanisi zaidi katika mwaka unaofuata.

Katika kikao hicho viongozi mbalimbali wamehudhuria akiwamo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni, Mkuu wa Jeshi la Polisi(IGP), Camillus Wambura, Mkuu wa Majeshi ya ulinzi, Jacobo Mkunda pamoja na viongozi wengine wa serikali na viongozi wa dini.