Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mabaki miili ya Watanzania kurudishwa nchini

Rais wa Ujerumani, Frank-Walter Steinmeier akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili Ikulu ya Dar es Salaam leo Oktoba 31, 2023. Pembeni yake ni Rais Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Muktasari:

  • Rais Samia Suluhu Hassan amedokeza uwezekano wa kurudishwa kwa mabaki ya miili ya Watanzania yaliyopo Ujerumani.

Dar es Salaam. Imechukua zaidi ya karne tangu mabaki ya miili ya Watanzania yahifadhiwe katika makumbusho mbalimbali nchini Ujerumani na sasa uamuzi wa kuyarejesha umefikia hatua nzuri.

Baadhi ya mabaki hayo ni yake ya miili ya machifu na viongozi mbalimbali waliokuwa vinara katika vita vya Tanganyika dhidi ya Ujerumani (Majimaji), mwaka 1905/07.

Hatua ya kurejeshwa kwa mabaki hayo, imedokezwa leo, Oktoba 31, 2023 na Rais Samia Suluhu Hassan alipozungumza na waandishi wa habari baada mazungumzo yake na Rais wa Jamhuri ya Ujerumani, Frank-Walter Steinmeier yaliyofanyika Ikulu ya Dar es Salaam.

Amesema miongoni mwa majadiliano aliyoyafanya na Rais huyo ni kuangalia uwezekano wa kurejesha mabaki ya miili ya Watanzania iliyopo nchini humo.

Mazungumzo hayo ni sehemu ya ratiba ya Rais Steinmeier aliyewasili nchini jana kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.

Amesema, "Najua kuna familia ambazo zinasubiri mabaki ya miili ya ndugu zao ambayo yapo kule katika makumbusho mbalimbali za Ujerumani, yote hayo tunakwenda kuyazungumza na kuona vipi tutakwenda nayo vizuri."

Katika hotuba yake mbele ya waandishi wa Habari, Rais Steinmeier naye ameeleza mpango huo, akidokeza unatarajia kufanyika kwa siku zijazo.

Amesema hilo litaambatana na kupeleka Ujerumani taarifa za hali za waathirika wa vita vya majimaji anaotarajia kukutana nao kesho.

Agizo la kurejeshwa kwa mabaki ya Watanzania yaliyopo Ujerumani, aliwahi kulitoa Januari 21, 2022 alipohutubia tamasha la machifu nchini.

Hata hivyo, Januari mwaka huu, aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Mohammed Mchengerwa alikutana na Balozi wa nchi hiyo, Rejine Hess kwa mazungumzo kuhusu hatua hiyo.