Macron ataka marekebisho makubwa Ulaya

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron
Muktasari:
- Macron, ambaye alifanya ziara yake ya kwanza nje ya nje ikiwa ni siku moja tu baada ya kula kiapo cha kushika madaraka, alitoa pendekezo hilo alipokutana na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel mjini hapa juzi kujadili na kuendeleza na kuimarisha uhusiano kati ya Ufaransa na Ujerumani, nchi mbili wanachama wa EU ambao unaonekana kukabiliwa na hali ya sintofahamu.
Berlin, Ujerumani. Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ametaka yafanyike marekebisho makubwa ndani ya Umoja wa Ulaya ili kuondokana na mgogoro unaoikabili kutokana na kupanda chuki.
Macron, ambaye alifanya ziara yake ya kwanza nje ya nje ikiwa ni siku moja tu baada ya kula kiapo cha kushika madaraka, alitoa pendekezo hilo alipokutana na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel mjini hapa juzi kujadili na kuendeleza na kuimarisha uhusiano kati ya Ufaransa na Ujerumani, nchi mbili wanachama wa EU ambao unaonekana kukabiliwa na hali ya sintofahamu.
Katika mazungumzo yao Macron amesema wamekubaliana kwa pamoja kufanya kazi ndani ya Umoja wa Ulaya kwa ukaribu zaidi.
Pia, Kansela Merkel alisema ilikuwa lazima kwa wazo la mabadiliko ya mikataba kwa ajili ya mageuzi ya Ulaya inayokabiliwa na mgogoro wa kupanda kwa chuki na ukabila. "Kwa mtazamo wa Ujerumani, inawezekana kubadili mikataba kama itakua ni muhimu," alisema Angela Merkel kwa vyombo vya habari mjini Berlin.
Macron alisema, "Suala la mabadiliko ya mkataba lilikuwa mwiko kwa Ufaransa, lakini katika utawala wangu halitakua mwiko."
Siku moja baada ya kutawazwa Macron alimteua mwanasiasa wa siasa za wastani, Edouard Philippe wa chama cha Republican kuwa waziri mkuu. Macron, kama walivyofanya watangulizi wake Nicolas Sarkozy na François Hollande, safari ya kwanza nje ya nje ilikuwa kuitembelea Ujerumani.