Madaktari bingwa waliofariki Arusha kizikwa Marangu na Njombe

Madaktari bingwa wafariki na kuacha simanzi Arusha

Arusha. Madaktari bingwa wawili waliofariki mapema wiki hii wanatarajiwa kuzikwa Marangu mkoani Kilimanjaro na Njombe.

Madaktari hao ambao vifo vyao vimeacha simanzi jijini Arusha niĀ  Dk Lamweli Henry Makando, mmoja wa wamiliki wa hospitali ya St Thomas ambaye alikuwa daktari bingwa na upasuaji na Dk Simon Kavavila daktari bingwa wa magonjwa ya watoto, wamefariki Jumatatu na Jumanne, baada ya kulazwa katika hospitali ya St Thomas na baadaye kukimbizwa hospitali ya KCMC.

Akizungumza na Mwananchi leo Machi 6, Dk Julius Msuya mmoja wa wamiliki wa hospitali ya St Thomas amesema Dk Makando anatarajiwa kuzikwa Jumatatu Machi 8, 2021 Marangu na Dk Kavavila atazikwa Njombe.

Kabla kukumbwa na kifo madaktari hapo, walikuwa wamelazwa pamoja katika hospitali ya St Thomas, akianza kuumwa Dk Kavavila na baadae Dk Makando.

Mkazi wa Arusha, Rehema Nelson amesema kufariki kwa madaktari hao ni pigo kubwakatika jiji la Arusha.

"Walikuwa ni tegemeo kubwa kwa wagonjwa wengi ndio sababu msiba wa umekuwa gumzo," amesema

Amesema watoto wengi waliugua wamepata matibabu ya Dk Kavavila aliyekuwa anatoa huduma katika hospitali mbalimbali lakini pia kwa akina mama wenye matatizo ya upasuaji walipata matibabu ya Dk Makando.

Mgaga Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Dk Widson Sichalwe alisema vifo vya madaktari hao vimesikitisha sana.