Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mafuriko yakumba kaya 100 Mbeya

Spika wa Bunge na Mbunge wa Mbeya mjini Dk Tulia Ackson akitembelea eneo lililokumbwa na mafuriko katika kata ya Uyole na kuwapa pole Wananchi.

Muktasari:

  • Zaidi ya kaya 100 mkoani Mbeya zimesombwa na mafuriko kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha na kusababisha uhaba wa makazi na chakula.

Mbeya. Spika wa Bunge na Mbunge wa Mbeya Mjini, Dk Tulia Ackson ametoa msaada wa chakula kwa kaya zaidi ya 100 zilizokumbwa na mafuriko Jumamosi Januari 7, mwaka huu kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha maeneo ya milimani.

Imeelezwa kuwa kati ya kaya hizo 20 zimekosa mahala pa kuishi kufuatia nyumba zao zilizojengwa kwenye mkondo wa maji kusombwa na mafuriko ikiwepo chakula, mavazi na kusababisha kukosa mahala pa kuishi.

Kufuatilia hali hiyo Spika Dk Tulia amewatembelea wananchi hao leo Jumatatu Januari 9, 2023 na kutoa msaada wa mchele kilo 800 maharage kilo 200 na kuhaidi kushirikiana na Serikali kutatua changamoto ikiwepo kuboresha miundombinu.

“Nilipata taarifa ya kuwepo kwa changamoto ya mafuriko katika Kata za Igawilo, Uyole, Iganjo na Iduda ambayo yameleta madhara makubwa ikiwepo baadhi ya kaya kukosa makazi sambamba na uharibifu ikiwepo vyakula na vitu vingine kusombwa na maji,” amesema.

Dk Tulia amesema kuwa ameguswa na changamoto hiyo iliyowakumba wananchi na kwamba atashirikiana na Serikali kuhakikisha wanaboresha miundombinu ili kuwezesha kupunguza athari kama hizo zisijitokeze tena

“Ndugu zangu niwape pole sana kwa haya maswahibu yaliyowakuta, niwahakikishie Serikali yenu tukufu ipo nanyi katika kipindi hiki na nimeongea na Mheshimiwa Waziri Mkuu kumuelezea haya na amenihakikishia kwamba watakuja kufanya tathimini ili kuona hatua ya kufanya ili kukabiliana na janga hili,” amesisitiza Dk Tulia.

Awali akimkaribisha Dk Tulia, Diwani Kata ya Uyole, Daniel Mwashidiga amesema kuwa maji yaliyosababisha mafuriko yalitokana na mvua kunyesha milimani na kupelekea kukosa mwelekeo na kuzingira makazi ya kaya zaidi ya 100 zenye wakazi 300 huku 20 kukosa makosa makazi

“Mvua ilinyesha mlimani huku hali ya hewa ilikuwa nzuri ilikuwa majira ya saa 11 za jioni ghafla tukaona maji mengi yakiwa na kasi ya ajabu ambayo yalizingira makazi na kuleta uharibifu,” ameseme.

Aidha amesema kuwa idadi kubwa ya kaya ambazo makazi yao yalibomoka ni ambao wamejenga kwenye mifereji ya mkondo wa maji ya mvua na katika hilo anaomba Serikali kuwaondoa ili kuepuka madhara ikiwepo kufanya maboresho ya kufanya mifereji

“Mimi ni mwanasiasa na hawa wananchi ni wapiga kura wangu, sasa inapotokea hali hii ni lazima nami sasa nivae sura nyingine lengo ni kuokoa wananchi, kwani mvua ingenyesha usiku leo tungekuwa tunazungumza masuala mengine,” amesema.

Amesema hiyo ni mara ya tatu kwa vipindi tofauti kwa eneo hilo kukumbwa na mafuriko katika msimu wa mvua na  anashangazwa  watu wanauziwa viwanja na kuendelea kujenga licha ya kuwa na changamoto hiyo.

Desemba 31, 2022 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera alitoa tahadharisha wananchi kuondoka kwenye maeneo yenye mikondo ya maji ikiwepo mabondeni kufuatia taarifa za Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA).