Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mahakama yamkalia kooni Rais Ruto, yamtaka atoe ushahidi

Muktasari:

  • Mahakama yamkalia kooni Ruto, yamshutumu kwa kuingilia uhuru wa mhimili huo. Jaji Mkuu amtaka kutoa ushahidi dhidi ya tuhuma za rushwa anazozielekeza kwa mhimili huo.

Dar es Salaam. Unaweza kusema Rais wa Kenya William Ruto ameanza mwaka vibaya kufuatia kutakiwa kutoa ushahidi wa kile alichodai    mhimili wa Mahakama nchini humo, unajihusisha na  vitendo vya rushwa na kuvuruga mipango ya Serikali.

Jaji Mkuu wa nchi hiyo, Martha Koome amevunja ukimya kufuatia tuhuma hizo na kumtaka Rais Ruto atoe ushahidi kuthibitisha madai hayo, yanayotoa taswira hasi kwa mhilimi huo wa haki.

Ruto ameutuhumu mhimili huo kuwa umekuwa ukizuia utekelezaji wa sera na sheria zilizopitishwa na Bunge, lengo likiwa kuvuruga mipango ya Serikali.

Jaji Martha ametoa changamoto kwa kiongozi huyo mkuu wa nchi kutoa ushahidi kuhusu madai ambayo aliibua dhidi ya maofisa wa mahakama, ambao hawakutajwa majina wanadaiwa kutumia maagizo ya mahakama kusitisha miradi ya Serikali.

Ukumbi ule ule ambapo yeye na majaji wengine wa Mahakama ya Juu zaidi kwa kauli moja waliidhinisha ushindi wa Ruto, Jaji Martha aliutumia kama jukwaa la kumtaka  kiongozi huyo mkuu wa nchi  na viongozi wa Kenya Kwanza waliochukizwa na kile wanachodai mahakama kukwamisha miradi ya Serikali  watoe ushahidi wa wanachokisema.

Mwanasheria huyo nguli amesema Tume ya Huduma za Mahakama (JSC) ambayo anaiongoza ina uwezo wa kushughulikia malalamiko yote dhidi ya maofisa wa chombo hicho cha haki.

“Tuko tayari kushughulikia malalamiko yoyote dhidi ya jaji au ofisa wa mahakama ambaye anahusishwa na ufisadi au kitendo kingine chochote cha utovu wa nidhamu. Hata hivyo, malalamiko hayo lazima yatolewe na kushughulikiwa kwa njia iliyoainishwa na Katiba. Siku zimepita ambapo maofisa walifukuzwa ofisini kwa kutajwa majina,” amesema.

"JSC, ambayo ni chombo kilichoidhinishwa na Katiba kushughulikia masuala ya malalamiko, itachukua hatua tu kwa msingi wa ushahidi na si kwa taarifa za kawaida au madai ambayo hayajathibitishwa," ameongeza.

Mbali na msimamo huo Jaji Martha alitumia jukwaa hilo kutoa wito kwa majaji na watumishi wa Mahakama kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa viapo vyao vya kazi,  kwa mujibu wa sharia, bila woga wa vitisho na bila upendeleo wowote.