Mahakama yatupa mapingamizi kesi ya Mbowe, wenzake

Mahakama yatupa mapingamizi kesi ya Mbowe, wenzake

Muktasari:

  • Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi leo Jumatano Oktoba 20, 2021 imetupilia mbali pingamizi la kwanza kwamba maelezo ya mshtakiwa wa pili Adamu Hassan Kasekwa yaliandikwa nje ya muda.


Dar es Salaam. Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi leo Jumatano Oktoba 20, 2021 imetupilia mbali pingamizi la kwanza kwamba maelezo ya mshtakiwa wa pili Adamu Hassan Kasekwa yaliandikwa nje ya muda.

Vile vile  imekataa hoja ya pili kuwa Adamu Kasekwa aliteswa kwani hakutatolewa ushahidi huo. Hivyo maelezo yalitolewa na mshtakiwa wa pili kwa ridhaa yake.

Uamuzi huo umetolewa katika kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu.

Akisoma uamuzi huo Jaji Mustapha Siyani ameeleza kuwa anakubaliana na Jamhuri kuwa mazingira yaliyokuwepo yana mantiki kuwa walikuwa wakiendelea na upelelezi.

Amesema kuchelewa kuhojiwa kwake kulikuwa na sababu za kisheria chini ya kifungu cha 51(1) Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai.