Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Majaliwa ahamasisha maombi kwa Yanga ishinde fainali

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza bungeni alipokuwa akijibu maswali ya papo kwa hapo ya wabunge, katika kikao cha 37 cha mkutano wa Bunge la Bajeti, jijini Dodoma leo. Picha na Edwin Mjwahuzi

Muktasari:

  • Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameomba Watanzania kwa imani zao kuungana kwa ajili ya kuiombea timu ya Yanga ambayo inasafiri leo kuelekea Algeria.

Dodoma. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameomba Watanzania kwa imani zao kuungana kwa ajili ya kuiombea timu ya Yanga ambayo inasafiri leo kuelekea Algeria.

Yanga inasafiri leo Juni Mosi, 2023 kuelekea Algeria ambako itacheza fainali yake katika mzunguko wa pili Juni 3, 2023 baada Yanga kupoteza kwa mabao mawili kwa moja.

Leo Juni mosi, 2023 Majaliwa akijibu maswali ya nyongeza ya papo kwa hapo bungeni, amesema timu hiyo itaondoka kwa ndege kwenda kukamilisha mchezo wa pili wa fainali ya Kombe la Shiriko la Afrika.

“Mheshimiwa Spika, kabla ya kujibu maswali ya wabunge, leo timu yetu ya Dar Young Afrika itaondoka muda si mrefu uwanja wa ndege kuelekea Algeria, Watanzania kila mmoja kwa dini yake tuwaombee wakashinde,” amesema Majaliwa.

Amesema kuwa timu ya Yanga ina uwezo mkubwa na imani yake ni kuwa itarudi na ushindi katika ardhi ya Tanzania kwa ushindi wa magoli mengi.

Kiongozi huyo amesema kuwa bado kuna matumaini makubwa kuwa kombe la Shiriko kwa mara ya kwanza litakuja Tanzania kwani sababu na uwezo vipo.

Amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa ndege ambayo itasafiri na wachezaji pamoja na viongozi wa Serikali na mashabiki wachache kwamba kitendo hicho ni cha kizalendo ambacho lazima kiungwe mkono kwani timu hiyo inakwenda kuwakilisha.