Majaliwa ataka mshikamano shughuli ya kuwateketeza nzige

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa

Monduli. Waziri mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewataka Watanzania kushikamana katika kipindi hiki ambacho baadhi ya maeneo shughuli ya kuwateketeza nzige inaendelea, akiwataka wananchi kushirikiana na wataalam kuwaangamiza.

Majaliwa ameyasema hayo leo Alhamisi Machi 4, 2021 alipotembelea eneo la Engaruka  lililovamiwa na nzige wa jangwani waliotokea nchini Kenya.

Nzige hao walimwagiwa sumu jana usiku na leo asubuhi na helikopta ya shirika la kupambana na nzige wekundu la Zambia.

"Zoezi hili ni letu sote, twende nalo pamoja tuendeleze mapambano haya ya nzige maana hawa ni hatari sana kwetu, hatutataka watuvuruge na hatutawapa nafasi.”

"Tumejipanga vizuri kupambana maana wanazaliana mno hawafai kuachwa hata tone, Serikali tumekusanya kila tulichonacho kwa ajili ya mapambano ya kuwaangamiza na kuwateketeza wote,” amesema.

Majaliwa ambaye ni mbunge wa Ruangwa amesisitiza, “niwasihi Watanzania katika kipindi hiki ambacho tumeingiliwa na nzige tushikamane, nimefurahi sana wananchi mlivyojitokeza kusaidiana na wataalamu wetu dhidi ya mapambano ya nzige hawa.”

Mtendaji mkuu huyo wa Serikali  amewatahadharisha wananchi kutokula Waziri mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewataka Watanzania kushikamana katika kipindi hiki ambacho baadhi ya maeneo shughuli ya kuwateketeza nzige inaendelea, akiwataka wananchi kushirikiana na wataalam kuwaangamiza.nzige hao watakapowaona kwa kuwa wameshamwagiwa sumu.