Majaliwa atua Monduli kushuhudia shughuli ya kuteketeza nzige

Muktasari:

Waziri mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewasili katika eneo la Engaruka Wilaya ya Monduli mkoani Arusha lililovamiwa nzige wa jangwani walioingia nchini  wakitokea nchi jirani ya Kenya.

Monduli. Waziri mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewasili katika eneo la Engaruka Wilaya ya Monduli mkoani Arusha lililovamiwa nzige wa jangwani walioingia nchini  wakitokea nchi jirani ya Kenya.

Februari 19, 2021 Serikali ilitangaza uwepo wa kundi la nzige zaidi ya milioni 50  nchini wenye uwezo wa kuruka kilomita 80 kwa siku  ambapo hadi leo Alhamisi Machi 4, 2021 wameteketezwa katika Wilaya za Siha, Mwanga Longido na Simanjiro.

Walioambatana na Majaliwa ni Waziri wa Kilimo,  Profesa Adolf Mkenda na naibu wake, Hussein Bashe, maofisa wa wizara hiyo na wakuu wa mikoa,  Anna Mghwira (Kilimanjaro), Iddy Kimanta (Arusha)  na Joseph Mkirikiti (Manyara).

Nzige hao wanateketezwa kwa dawa inayosambazwa na helikopta ya taasisi ya kupambana na nzige wekundu yenye makao makuu nchini Zambia