Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Makada 19 Chadema wapandishwa kizimbani, wapata dhamana

Makada 19 Chadema wapandishwa kizimbani, wapata dhamana

Muktasari:

Viongozi na wanachama 19 wa Chadema leo Alhamisi wamefikishwa katika  mahakama ya hakimu mkazi Mkoa wa Mwanza  na kusomewa  shtaka la kufanya fujo kwenye mikusanyiko ya dini na kuachiwa kwa dhamana.

Mwanza. Viongozi na wanachama 19 wa Chadema leo Alhamisi wamefikishwa katika  mahakama ya hakimu mkazi Mkoa wa Mwanza  na kusomewa  shtaka la kufanya fujo kwenye mikusanyiko ya dini na kuachiwa kwa dhamana.

Akisoma shtaka hilo, Wakili wa Serikali, Bisela Bantulaki ameiambia Mahakama kuwa washtakiwa hao walitenda kosa hilo Agosti 15, 2021 katika Kanisa Katoliki Parokia ya Kawekamo wilayani Ilemela jijini hapa.


Bantolaki amedai kuwa washtakiwa hao baada ya kufika katika kanisa hilo walianza kufanya fujo wakati ibada ya matoleo ikiendelea.
Akizungumza mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Emmael Lukumay, Wakili wa upande wa utetezi, Paul Kiheja amedai kuwa kosa walilofanya watuhumiwa hao linadhaminika hivyo anaomba wapatiwe dhamana.

Soma zaidi:Polisi wavunja mkutano wa Chadema, 30 wakamatwa
Baada kusikiliza pande zote, Hakimu Lukumay ameagiza watuhumiwa hao kupewa dhamana kwa masharti ya kutoa dhamana ya mali kauli ya Sh1 milioni kila mmoja, kuwasilisha barua ya utambulisho kutoka ofisi ya Serikali ya Mtaa na nakala moja ya kitambulisho cha mpigakura au cha Taifa masharti ambayo waliyatimiza.


"Kwa sababu hakuna pingamizi kutoka upande wa Jamhuri, naagiza washtakiwa hawa wapewe dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana," amesema Bantulaki.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba 21 mwaka huu itakapotajwa tena.