Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Makarani wanaotembea na vishkwambi maeneo ya starehe waonywa

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mwenendo wa sensa mkoani humo. Picha na Janeth Joseph

Muktasari:

  • Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu amewataka makarani wa sensa mkoani humo kutokwenda na vishikwambi kwenye maeneo ya starehe.

Hai. Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu amewataka makarani wa sensa mkoani humo kuwa kutokwenda na vishikwambi kwenye maeneo ya starehe ili visiibwe na badala yake wavirudishe nyumbani baada ya kumaliza kazi zao.

Amesema serikali imetumia fedha nyingi kugharamia vifaa hivyo na kuwataka kuwa navyo makini.

Babu ametoa agizo hilo leo Agosti 24, 2022 akiwa wilayani Hai wakati akikagua mwenendo wa shuguli ya sensa inayoendelea hapa nchini.

"Makarani wa sensa mwe makini kwa sababu hivi vishikwambi ni gharama kubwa ambayo serikali imetumia, hivyo sio kwenda navyo sehemu za starehe.

“Hakikisheni mkimaliza navyo kazi mnakwenda kuvihifadhi nyumbani ndio wendelee na mambo yenu mengine," amesema.

Amesema mkoa huo unao ulinzi wa kutosha katika maeneo mbalimbali ili kuhakikisha makarani wanafanya kazi zao katika sehemu salama.