Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mama amchoma mwanaye mikono akimtuhumu kuiba Sh250

Mtoto mwenye umri wa miaka mitano akiwa amepakwa dawa ya kienyeji baada ya mama yake kumchoma moto akimtuhumu kudokoa dagaa na kuiba 250 katika kata ya Dihimba kiji Cha Namanjele. Florence Sanawa

Muktasari:

  • Mtoto wa miaka mitano amechomwa moto mikononi na mama yake baada ya kudokoa dagaa na kuiba Sh250 nyumbani kwao.

Mtwara. Mkazi wa Kijijii cha Namanjele mkoani Mtwara, Somoe Mohamed amemchoma mikono mtoto wake mwenye umri wa miaka mitano kwa madai ya kudokoa mboga na kuiba Sh250.

Akizungumza na Mwananchi kijijini hapo leo Oktoba 4, Somoe amekiri kufanya ukatili huo, akisema lengo lake lilikuwa ni kumwadhibu mtoto kwa tabia mbaya aliyoonyesha

"Nilikuwa namwadhibu kwa tabia yake. Siku ya kwanza alichukua Sh50 na siku ya pili alichukua Sh200 na baadaye akaanza kudokoa dagaa nikamuonya, lakini hakusikia mpaka sasa mtoto anasiku tatu tangia amechomwa moto,” amesema.

Baba wa mtoto huyo, Juma Lubega amesema kuwa yeye alisikia kuwa mwanaye amechomwa moto na mama ake hakuamini lakini alipofika nyumbani alimuona mtoto akiwa ameungua sehemu ya mikono yake vikiwemo vidole.

“Nilisikia uchungu kama baba nilipouliza nikaamibiwa kuwa kaiba Sh250 na kudokoa dagaa, yaani inaonyesha kuwa alimfunga kamba mikononi akaweka nyasi akamchoma mtoto na inaonyesha alipowasha moto aliondoka ndio maana mtoto amepata madhara makubwa,” amesema Lubega.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kijiji hicho, Mussa Mkadimba amesema kuwa tukio hilo sio zuri kwakuwa halifundishi mtoto bali linaweza kumfanya akawa katili.

“Nimelipokea vibaya hili jambo kwakuwa halikuletwa kwangu nilisikia niliamua kulifatilia mwenyewe ili kuona kuna ukweli kiasi gani nikakuta ni kweli mtoto ameunguzwa na moto kwa maeneo ya mikoa yake.

“Huyu mtoto tangia uchomwe hajapelekwa pelekwa hosptiali yoyote wala hapata dawa zaidi ya miti shamba wanayotumia kumuwekea mikononi kutookana na imaini kuwa atapona kwakutumia dawa za asili,” amesema.

Kwa upande wake Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, ACP Nicodemus Katembo alipoulizwa na mwananchi kuhusu tukio hilo alisema kuwa yuko safarini na akifika atalifatilia na kulitolea maelezo.