Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mama, wanawe wawili wateketea kwa moto Shinyanga

Muktasari:

Watu watatu wamefariki dunia wakiwa ndani ya nyuma baada ya kuungua moto usiku wa kuamkia leo Jumatano, Novemba 30, 2022 wilayani Kahama mkoani Shinyaga wakati wakiwa wamelala nyumbani kwao huku chanzo cha moto huo kikiwa hakijajulikana.

Shinyanga. Watu watatu wamefariki dunia wakiwa ndani ya nyuma baada ya kuungua moto usiku wa kuamkia leo Jumatano, Novemba 30, 2022 wilayani Kahama mkoani Shinyaga wakati wakiwa wamelala nyumbani kwao huku chanzo cha moto huo kikiwa hakijajulikana.


Tukio hilo limethibitishwa na Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya ya Kahama, Festo Kiswaga na kuwataja waliopoteza maisha ni pamoja na Dotto Juma (32) ambaye ni mama mzazi na watoto wake, Samsom Mathew (13) na Joseph Samson (9)


Kiswaga amesema tukio hilo limetokea alfajiri wakiwa wamelala ndani ya nyumba yao, moto huo uliwaka na kuwaunguza hali iliyosababisha kupoteza maisha huku Jeshi la Zimamoto na Uokoaji likifanikiwa kuuzima moto huo.


Amesema waliopoteza maisha ni mama yao mzazi na watoto wake wawili waliokuwa wanasoma shule ya msingi Athony wa Padua, darasa la pili na la sita na kuiomba familia hiyo kuwa watulivu wakati Serikali ikiendelea na uchunguzi.


Nao baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo akiwemo mwenyekiti wa Nzengo ya Miembeni, Athony kitambi aliiomba Serikali kutoa elimu ya kukabiliana na majanga ya moto.


“Tunaliomba jeshi la zimamoto na ukoaji litoe elimu kwa wananchi juu ya kujikinga na majanga ya moto yanayojitokeza mara kwa mara katika mkoa wa Shinyanga, wiki moja wamepoteza maisha wanafunzi watatu leo wawili na mtu mmoja hii si kawaida," alisema Kitambi.


Tukio hilo ni la tano la nyumba na mabweni kuungua moto  katika mkoa wa Shinyanga ambayo yamesababisha vifo kwa watu sita ndani ya Novemba mwaka huu