Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mambo ni motomoto kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2022 Kenya

Muktasari:

Muda huo ulishuhudia vita vya maneno kati ya kambi ya Ruto na ile ya Rais Uhuru

Nilisema miaka minne iliyopita katika jukwaa hili kwamba Naibu wa Rais wa Kenya, William Ruto angetemwa na Rais Uhuru Kenyatta wakati mmoja. Ubashiri huo sasa umetimia na mambo si mazuri katika upande wa Ruto na wafuasi wake.

Baada ya mwezi mmoja wa uhasama katika chama tawala cha Jubilee, kuna juhudi za kutafuta uwiano na umoja katika chama cha Jubilee.

Muda huo ulishuhudia vita vya maneno kati ya kambi ya Ruto na ile ya Rais Uhuru. Wafuasi wa Makamu wa Rais kama vile Seneta Kipchumba Murkomen hajaficha hisia zake kuhusu anachofikiria katika vita baridi katika chama cha Jubilee.

Akizungumza katika runinga moja ya kitaifa, Murkomen anasema Ruto anapigwa vita na watu wanaomzunguka Rais Uhuru.

Ingawa hakutaja majina, mwanasiasa huyo anasema watu hao ambao hawataki kumuona Ruto akimrithi Rais Uhuru wanajulikana.

Duru za kuaminika zasema kwamba, kambi ya Ruto zinawanyoshea kidole cha lawama mshauri wa Rais, Nancy Gitau na Katibu wa Wizara ya Masuala ya Ndani, Ikara Kibicho miongoni mwa wengine. Wawili hao wana uhusiano wa karibu na Rais Uhuru.

Matamshi ya Murkomen yalipanua kidonda sugu kinachoendelea kuumiza Jubilee na kusababisha uhasama zaidi huku vita dhidi ya ufisadi ukiendelea kuibua hisia mseto miongoni mwa wana jubilee.

Upande wa Ruto unaona vita dhidi ya ufisadi kama mpango wa kambi ya Rais Uhuru kumlenga Ruto lakini hayo yamevutia pia shutuma kutoka katika pembe tofautitofauti.

Wachambuzi wa siasa wanahoji kwa nini wafuasi wa Ruto wanalalamika na kuwa na wasiwasi mkubwa kuhusu sera hii mpya ya kuchunguza mali za wanasiasa na viongozi wengine ili kujua walijilimbikizia mali kivipi.

Kinachowauma

Lakini kama Ruto alijitajirisha kwa jasho lake mbona yeye na wafuasi wake wagubikwe na wasiwasi? Je, wanaogopa nini? Wanafaa kuwaambia Wakenya kwa nini wanapinga mchakato huu wa mali yao na wengine kuchunguzwa.

Wasiwasi wao unadhihirisha kwamba huenda kuna kitu wanakificha na wanahofia kufichuliwa.

Matamshi ya Murkomen yanababaisha kuwa Jubilee, hasa wabunge na maseneta wa jamii ya Kalenjin ambayo ni kabila lake Ruto, ilikuwa vyema kufanya mkutano wa dharura kuokoa mustakabali wao na kuonekana kama wenye kutafuta amani wala si wenye kupanda mbegu ya uadui. Wabunge na maseneta wote Wakalenjin walikutana kwa saa tano katika hoteli ya kifahari ya Weston Jijini Nairobi siku chache zilizopita kutafuta jinsi ya kumaliza uhasama katika chama chao na kufanya kazi pamoja.

Mkutano huo mrefu ulizaa matunda. Wakihutubia wanahabari baada ya kumaliza mkutano huo, wanasiasa hao walisema waliafikiana kuzika tofauti zao na kufanya kazi pamoja kama zamani.

Walisema, kinyume na habari kwamba Jubilee imesambaratika, kila kitu kiko shwari chamani. Lakini Wakenya si wajinga. Wana akili zao na wanajua kwamba hakuna amani katika chama hicho kinachotawala.

Rais Uhuru hajawahi ficha hisia zake dhiki ya makamu wake kwa muda wa wiki kadhaa. Siku hizi, Rais amesahau jina la Ruto na kila anapozungumza kumuhusu anamtaja kama “huyu” ama “yule jamaa wa kutangatanga.”

Duru ambazo hazijathibitishwa zinaarifu kwamba kuna mpango wa kuwatimua viongozi wa walio wengi katika Bunge la Kitaifa na Seneti. Murokemen na Aden Duale sasa wamo katika njia panda. Hawajui kama kazi kama viongozi wa walio wengi katika Seneti na Bunge mtawalia ziko salama.

Wabunge wa Jubilee ambao sasa wanaweza kuwategemea wabunge wa upinzani kushirikiana nao wanapokuwa na mswada au hoja ya kupitisha, wana nguvu kubwa wa kutimiza mpango huu.

Hii ni kufuatia salamu kati ya Rais Uhuru na kiongozi wa upinzani Raila Odinga. Tangu Machi 9 ambapo salamu hizo zilifanyika kati ya viongozi hao, kumekuwa na hali ya utulivu nchini hadi wakati mizozo ilitisha kusambaratisha Jubilee.

Duale na Murkomen wanatuhumiwa na wanasiasa wa Jubilee kwa kukosa kudhihirisha kwamba nyadhifa zao hazifai kupendelea kambi yoyote katika Jubilee. Kisheria, viongozi wa walio wengi katika Bunge na Seneti ni nguzo muhimu ya chama na serikali.

Wawili hao wanafaa kuwa wanaunga mkono kwa dhati sera za serikali lakini kinyume na majukumu yao, viongozi hao wamekuwa vipofu kwa sababu ya ukereketwa wao kwa Makamu wa Rais. Wamesahau majukumu yao na kuweka mbele tamaa ya uongozi wa mwaka wa 2022.

Mienendo yao haikuwaudhi tu Wakenya bali baadhi ya viongozi wa jamii ya Wakalenjin ambao walifanya mkutano na wanahabari kuwazomea.

Mbunge wa Cherang’any, Joshua Kuttuny na mwenzake wa Nandi Hills Alfred Keter waliwaonya wanasiasa wa mrengo wa Ruto wakiwaambia wakome kuropoka na kutoa matamshi yanayoweza kuleta mizozo nchini.

Hii ilikuwa baada ya wabunge wa mrengo wa Ruto kumuhusisha Mamake Rais Uhuru Mama Ngina Kenyatta na visa vya ufisadi vilivyokithiri. Vilevile, wabunge hao walimuhusisha nduguye Uhuru Muhoho Kenyatta na sakata linaloendelea la sukari yenye zebaki iliyoagizwa kutoka Brazil.

Hivi majuzi, Rais Uhuru alisema kwamba ikiwa ndugu yake aliagiza sukari kama ilivyodaiwa na wanasiasa wa Ruto, basi hapatakuwa na lingine ila kumwadhibu.

Lakini Waziri wa Kilimo, Mwangi Kiunjuri amemtetea vikali Muhuho akisema kampuni yake ya Protech Limited haiko kwenye orodha ya waagizaji wa sukari. Aliongeza kwamba Muhoho alikuwa ametuma ombi la kupewa idhini ya kuagiza bidhaa hiyo lakini hakukubaliwa.

Kiunjuri aliapa kuwaadhibu wote walioingiza jina la Muhoho kwenye orodha ndefu ya wafanyabiashara walioagiza sukari duni inayohatarisha maisha ya wananchi.

Matamshi kutoka mrengo wa Ruto ni juhudi za mafisadi fulani wanaojaribu kusambaratisha vita dhidi ya ufisadi. Lakini je, umeshashuhudia ng’ombe akizuiwa na kelele za chura kunywa maji?

Raila hajaachwa na wanasiasa wa mrengo wa Makamu wa Rais. Hakuna siku wamekosa kumtaja kiongozi huyo wakimlaumu kwa mabomu yanayolipuka kila wakati ndani ya chumba cha chama kinachotawala.

Wanachokosa kutambua kwamba wanasiasa hao ni kwamba, Raila si kiini cha matatizo yao. Wanafaa kutafuta kiini cha shida zao ndani ya chama chao. Haitasaidia kumrushia mawe Raila kila wakati badala ya kulegeza darubini yao kwa marafiki wao katika Jubilee.

Vita vya Jubilee vimeathiri mikutano iliyokuwa imepangwa kati ya wazee wa jamii ya Kikuyu na wenzao wa Kalenjin kumsaidia Ruto kuafikia maazimio yake ya kisiasa.

Mikutano kati ya wazee hao sasa yameahirishwa hadi wakati usiojulikana.

Wazee wa jamii ya Kikuyu ambayo ni kabila la Rais Uhuru sasa wanamtaka Ruto asahau kabisa urais mwaka wa 2022. Walimshauri Ruto astaafu na Rais Uhuru mwaka huo ili kutoa nafasi kwa viongozi wengine.

Huku uhusiano kati ya Uhuru na naibu wake ukiendelea kudorora, kiongozi wa nchi ameendelea kushirikiana na Raila katika ujenzi wa taifa.

Hivi karibuni Uhuru na Raila watafanya mkutano na Rais John Magufuli nyumbani kwa Raila katika eneo la Bondo.

Wale wana fikra finyu kwamba Uhuru na Raila wataachana hivi karibuni wanajidanganya. Uhuru amepata nguvu zaidi za kukabiliana na utovu wa nidhamu na ufisadi katika serikali yake baada ya kuzika tofauti zake na Raila.

Sasa ni kazi tu kati yao huku Ruto na wenzake wakitangatanga kutafuta kura za 2022. Jamani, 2022 ni miaka minne unusu kuanzia sasa. Kwa nini Ruto na wafuasi wake wasiangazie maendeleo badala ya kupoteza muda wao bure?