Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mashahidi 24 vielelezo 19 kesi ya Mbowe na wenzake

Muktasari:

  • Mashahidi 24 na vielelezo 19, wanatarajia kutoa ushahidi katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na wenzake watatu.

Dar es Salaam. Mashahidi 24 na vielelezo 19, wanatarajia kutoa ushahidi katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na wenzake watatu.

Miongoni mwa mashahidi hao, yupo aliyekuwa Mkurugenzi wa Upelelezi na Makosa ya Jinai nchini (DCI), Robert Boaz.

Ulinzi mkali Mbowe na wenzake wafikishwa Mahakamani Kisutu

Hayo yameelezwa leo, Agosti 23, 2021 na upande wa mashtaka ukiongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Nassoro Katuga akisaidiana na Ester Martin, wakati wakiwasomea maelezo ya mashaidi na vielelezo (Commital Proceedings) washtakiwa hao, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Thomas Simba.