Maswali kadhaa kuhusu matumizi ya gari na majibu yake

Wengi wetu hutumia magari kuendesha au kwa shughuli za kibiashara lakini huenda hatujui mambo fulani muhimu kuyahusu.

Lakini yapo mambo ambayo labda ushawahi kuyasikia kuhusu magari lakini ukashindwa kupata majibu. Katika makala haya kuna maswali muhimu kuhusu matumizi ya magari na majibu yake.


Je, matairi yanapaswa kubadilishwa bila gari kutumika?

Ndiyo. Iwe tunatumia gari au la, tunahitaji kubadilisha matairi kila baada ya miaka mitatu au minne. Na hivyo basi hakutakuwa na ajali za kupasuka kwa matairi.

Tairi inapaswa kuwa na uwezo wa kuhimili ongezeko la shinikizo lakini matairi ambayo yametumika kwa miaka mitatu hadi minne hayawezi kuchukua ongezeko hilo kama mapya.


Kitufe cha tahadhari kinapaswa kuwashwa muda gani

Kitufe cha hatari (chenye umbo la pembetatu) ni cha kawaida katika gari lolote. Kinapaswa kutumika tu katika hali ya hatari na vituo vya dharura vya barabarani kutokana na kuchomwa.

Lakini watu wengi hukitumia hata wanaposimama kwenye eneo la makutano. Ikiwa unatumia kitufe hichi wakati wowote kipaumbele chake kitapotea.

Taa nne za kitufe hichi hatari zitawashwa na kuwaka. Kwa hili, mtu akiona gari atajua kwamba tuko hatarini. Kinapaswa kutumika tu kwa nyakati muhimu zaidi.


Je manukato yanaweza kutumika kwenye gari?

Manukato yana kiasi kidogo cha vilevi (alcohol). Wakati wa kusafiri kwa gari, oksijeni ndani huwa ni kidogo. Ikiwa kuna manukato kemikali yake ina uwezekano wa kusababisha matatizo ya afya kwa wale ambao wana matatizo ya kupumua ndani ya gari.

Aidha, gari lina vipengele vyote vya umeme. Ikiwa kuna moto, manukato yataifanya kuwa mbaya zaidi. Ndiyo sababu ni bora kutotumia manukato.


Nini cha kufanya wakati wa ukungu?

Wakati wa baridi, mabadiliko ya hali ya hewa hutokea ghafla ikiwemo mvua. Kwa nyakati hizo, tofauti kati ya joto ndani ya gari na la nje husababisha ukungu kwenye kioo cha mbele na nyuma.

Ili kuuondoa washa kiyoyozi (AC) kwa muda. Kufanya hivyo kutaondoa ukungu haraka. Ikiwa unaendesha gari katika hali ya hewa kama hiyo, unaweza kushusha kioo kidogo ili kuzuia ukungu.


Nini kifanyike ili kupunguza joto kwenye gari?

Joto hupanda kwenye gari lililoegeshwa kwenye jua. 'Madirisha makubwa' yanapaswa kufunguliwa kabla ya kuondoka kwenye gari.

Hiyo ni ikiwa unafungua mlango wa kushoto mbele na mlango wa kulia nyuma na kuicha wazi kwa muda joto lote ndani litaondoka. Mbinu hii inafanya kazi vizuri.

Pia, kabla ya kuwasha injini ya gari, shusha vioo na uendeshe kwa angalau nusu kilomita na uwashe kiyoyozi, wakati huo huo ili joto ndani litoke.


Je, gari halipaswi kuzimwa gafla linapofika mwisho wa safari?

Ikiwa unapaswa kuzima gari baada ya kusafiri zaidi ya kilomita 50, usilizime kwa gafla. Injini lazima iendelee kufanya kazi kwa dakika mbili hadi tatu na kisha kuzimwa.

Kwa sababu hata wakati huo, kutokana na hali ya joto katika gari, chaja za turbo na vifaa vingine ndani ya gari haviwezi kurudi katika hali yake ya kawaida mara moja.

Ndio maana unapaswa kutoa muda kwake kurudi katika hali ya kawaida na kisha kuzima injini ya gari. Hapo ndipo mafuta kwenye injini yatarudi katika hali yake ya kawaida na vilainishi vitafanya kazi vyema.