Matokeo Sensa yabainisha huduma za jamii kuwa mbali na watu

Kamisaa wa Sensa ya watu na Makazi ya mwaka 2022 Anna Makinda (kulia) akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanal Ahmed Abbas (wapili kulia) wakifatilia mafunzo ya matumizi ya matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 kwa Mkoa wa Mtwara. Picha na Florence Sanawa

Muktasari:

  • Kamisaa wa Sensa ya watu na Makazi ya mwaka 2022 Anna Makinda amesema kuwa katika zoezi la Sensa ya Watu na Makazi maeneo mengi yalionyesha uwepo wa watu lakini huduma za kijamii kuwekwa mbali na watu bila kujali ongezeko la watu hali ambayo ni hatari kwao ambapo kwa mkoa wa mtwara kuna ongezeko la asilimia 3.3.

Mtwara. Mkoa wa Mtwara umetakwa kuwa na ongezeko kubwa la watu ambapo idadi ya watu wote ni 1,634,947 wanawake wakiwa ni 858,165 na wanaume 776,782 wenye umri wa kufanyakazi kati ya 15-64 wako 952,27 sawa na asilimia 58.2.

 Kauli hiyo ameitoa Kamisaa wa Sensa ya watu na Makazi ya mwaka 2022 Anna Makinda wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya matumizi ya matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 kwa mkoa wa Mtwara.

“Mfano utaona mtaa una watu wengi lakini hakuna huduma za jamii yaani shule, hospitali wala umeme yaani wanatembea zaidi ya kilomta mbili kufata huduma kupitia sense hii tuangalie mapungufu na kuyarekebisha,” amesema.

“Kwa mkoa wa Mtwara watu wameongezeka na  tumezidi idadi ya taifa asilimia 3.3 mtwara mmeongezeka na sasa mko zaiid ya milioni ni jambo zuri kwakuwa kuongezeka sio tatizo mkishaongezeka alafu?” amehoji.

“Hizi takwimu msipoangalia zitawachonganisha tukubali kuwa tulishakosea na sasa tuangalie asiwepo mtu wa kuachwa nyuma pale ambapo paplikuwa hakuna huduma sasa huduma ziende sio kwaajili ya mtu lakini tunaamini kuwa takwimu hizi zitakuja kuzalisha,” amesema.

“Huu mkoa unautajiri mkubwa ardhi kubwa haijatumika mnatumiaje kwaajili ya maendeleo ya nchi kama tunaongezeka uchumi inabidi ukue mara tatu ya idadi ya watu unaowahudumia,” amesema.

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanal Ahmed Abbas alisema kuwa katika maandalizi ya bajeti ya mwaka 2023/24 mkoa umezingatia matokeo ya sensa ya mwaka 2022 yametusaidia kupanga maendeo ya mkoa kwa uwiano wa idadi ya watu na mahitji yao ningependa kuzingatia umuhimu wa ili kujifunza vyema na kuongeza maarifa.

Akisoma taarifa kwa niaba ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dk Albino Chuwa, Tamali William alisema kuwa matokeo ya sensa bado yanaendelea kuchakatwa.

 “Katika matokeo ya tambuzi hizo hayajafanyiwa uchambuzi kufahamu idadi yao na wasiokuwa watanzania waliomo nchini kwakuwa wote wanahitaji huduma,” amesema.